Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 7:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 Maana ilipendeza sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii, aliye mtakatifu, asiokuwa na uovu, asiokuua na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Basi, ilikuwa jambo la kufaa sana kwetu kuwa na kuhani kama huyo, mtakatifu, asiye na hatia wala dhambi ndani yake; ametenganishwa mbali na wenye dhambi, na ameinuliwa juu ya mbingu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Basi, ilikuwa jambo la kufaa sana kwetu kuwa na kuhani kama huyo, mtakatifu, asiye na hatia wala dhambi ndani yake; ametenganishwa mbali na wenye dhambi, na ameinuliwa juu ya mbingu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Basi, ilikuwa jambo la kufaa sana kwetu kuwa na kuhani kama huyo, mtakatifu, asiye na hatia wala dhambi ndani yake; ametenganishwa mbali na wenye dhambi, na ameinuliwa juu ya mbingu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Kwa kuwa ilitupasa tuwe na Kuhani Mkuu wa namna hii, yaani aliye mtakatifu, asiye na lawama, asiye na dosari, aliyetengwa na wenye dhambi na kuinuliwa juu ya mbingu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Kwa kuwa ilitupasa tuwe na Kuhani Mkuu wa namna hii, yaani, aliye mtakatifu, asiye na lawama, asiye na dosari, aliyetengwa na wenye dhambi na kuinuliwa juu ya mbingu.

Tazama sura Nakili




Waebrania 7:26
39 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana alijua ya kuwa wamemtoa kwa husuda.


Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.


Malaika akajibu, akamwambia, Roho Mtakatifu atakujia, na nguvu zake Aliye juu zitakutilia kivuli: kwa biyo kitakachozaliwa kitakwitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.


Nae akawaambia marra ya tatu, Kwani? ubaya gani alioutenda huyu? sikuona hatta neno kwake la kustahili kufa; bassi nikiisha kumrudi nitamfungua.


Na sisi kweli ina haki; kwa maana sisi tunalipwa ijara ya haki ya matendo yetu: bali huyu hakutenda neno lisilofaa.


Akida alipoona lililokuwa, akamtukuza Mungu, akisema, Kwa kweli mtu huyu alikuwa mwenye haki.


Haikumpasa Kristo kupata mateso haya, ndipo aingie enzini mwake?


Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, na ndivyo ilivyompasa Kristo kuteswa, na kufufuka siku ya tatu;


Sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana mkuu wa ulimwengu anakuja, wala hana kitu kwangu:


Nae aliyenipeleka yu pamoja nami; Baba hakuniacha peke yangu: kwa sababu mimi nafanya siku zote yampendezayo.


Ninyi mlimkana yule Mtakatifu, yule Mwenye haki, mkataka mpewe muuaji:


Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika juu ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,


Maana alimfanya yeye asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili vefu, illi sisi tuwe haki ya Mungu katika Yeye.


Yeye kwa kuwa ni mwanga wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivitengeneza vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya peke yake utakaso wa dhambi zetu, aliketi juu mkono wa kuume wa ukuu;


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


Kwa kuwa ilimpasa veye, ambae kwa ajili yake na kwa kazi yake vitu vyote vimekuwa, akileta wana wengi hatta utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokofu wao kwa mateso.


Kwa hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, illi afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.


KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,


Bassi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi: (maana watu wale waliipata sharia kwa huo) kulikuwa na haja gani tena kuhani mwingine aondoke, wa daraja la Melkizedeki, wala si kwa daraja la Haruni?


BASSI, katika hayo tuuayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunae kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu mbinguni,


bassi si zaidi damu yake Kristo, ambae kwamba kwa Roho ya milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo mawaa, itawasafisheni dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hayi?


bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana kondoo asio na ila, na asio na waa, ya Kristo,


yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake;


alioko mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zimetiishwa chini yake.


nae ni kipatanisho kwa dhambi zetu: wala si kwa dhambi zetu tu, bali kwa dhambi za ulimwengu wote.


Na mnajua ya kuwa yeye alidhihiri, illi aziondoe dhambi zetu; na dhambi haimo ndani yake.


Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Filadelfia andika; Haya ayanena yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daud, mwenye kufungua wala hapana afungae, nae afunga wala hapana afuuguae.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo