Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 7:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 (kwa maana sharia ile haikukamilisha neno); na pamoja na haya kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwayo twamkaribia Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Maana sheria ya Mose haikuweza kukamilisha jambo lolote. Lakini sasa, mahali pake pamewekwa tumaini lililo bora zaidi ambalo kwalo tunaweza kumkaribia Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Maana sheria ya Mose haikuweza kukamilisha jambo lolote. Lakini sasa, mahali pake pamewekwa tumaini lililo bora zaidi ambalo kwalo tunaweza kumkaribia Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Maana sheria ya Mose haikuweza kukamilisha jambo lolote. Lakini sasa, mahali pake pamewekwa tumaini lililo bora zaidi ambalo kwalo tunaweza kumkaribia Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 (kwa maana sheria haikufanya kitu chochote kuwa kikamilifu). Kwa upande mwingine, tumeletewa tumaini lililo bora zaidi ambalo linatuleta karibu na Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 (kwa maana sheria haikufanya kitu chochote kuwa kikamilifu). Kwa upande mwingine, tumeletewa tumaini lililo bora zaidi ambalo linatuleta karibu na Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili




Waebrania 7:19
29 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa, neema na kweli zilikuwa kwa mkono wa Yesu Kristo.


Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.


na kwa huyu killa amwaminiye huhesabiwa kuwa hana khatiya katika mambo yale asiyoweza kuhesabiwa kuwa hana khatiya kwa torati ya Musa.


kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo tunasimama ndani yake; na twafurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.


Tusemeje, bassi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalijua dhambi illa kwa sharia: kwa maana singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.


Maana yale yasiyowezekana kwa sharia, kwa kuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa ajili ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili:


tukijua ya kuwa mwana Adamu hafanyiziwi wema kwa matendo ya sharia, hali kwa imani ya Yesu Kristo, sisi tulimwamini Yesu Kristo illi tufauyiziwe wema kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sharia; maana kwa matendo ya sharia hapana mwenye mwili atakaefanyiziwa wema.


Bassi, torati haipatani na ahadi za Mungu? Hasha. Kwa kuwa, kama ingalitolewa sharia iwezayo kuhuisha, yakini haki ingalipatikana kwa sharia.


Na hivyo sharia imekuwa mwalimu wa kutuleta kwa Kristo, illi tufanyiziwe wema kwa imani.


Katika yeye tuna ajasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya imani yake.


ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu;


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Bwana Yesu Kristo, tumaini letu;


BASSI kwa kuwa torati ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo, kwa dhahihu zile zile wanazozitoa killa mwaka daima, hawawezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.


kwa kuwa Mungu ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, illi wasikamilishwe pasipo sisi.


Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu ampendezae Mungu lazima aamini kwamba yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.


bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba yake; ambae nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na kujisifu kwetu, kwa kutumaini mpaka mwisho.


Bassi na tukikaribie kiti cha neema kwa nthubuitifu, illi tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.


illi kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu bawezi kusema nwongo, tupate faraja lililo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;


Bassi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi: (maana watu wale waliipata sharia kwa huo) kulikuwa na haja gani tena kuhani mwingine aondoke, wa daraja la Melkizedeki, wala si kwa daraja la Haruni?


Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo,


Nae, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye; maana yu hayi siku zote illi awaombee.


Lakini sasa amepata khuduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mtengenezaji wa agano lililo bora, lililoamriwa kwa ahadi zilizo bora na kuzitegemea.


Hii ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhahihu zinatolewa, zisizoweza kumkamilisha mtu aabunduye dhamiri yake,


Mkaribieni Mungu, nae atsiwakaribieni ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, kaisafisheni mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo