Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 7:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 asiyekuwa kuhani kwa sharia ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na kikomo:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Yeye hakufanywa kuhani kwa sheria na maagizo ya kibinadamu, bali kwa nguvu ya uhai ambao hauna mwisho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Yeye hakufanywa kuhani kwa sheria na maagizo ya kibinadamu, bali kwa nguvu ya uhai ambao hauna mwisho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Yeye hakufanywa kuhani kwa sheria na maagizo ya kibinadamu, bali kwa nguvu ya uhai ambao hauna mwisho.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 yeye ambaye amefanyika kuhani si kwa misingi ya sheria kama ilivyokuwa kwa baba zake, bali kwa misingi ya uwezo wa uzima usioharibika.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 yeye ambaye amefanyika kuhani si kwa misingi ya sheria kama ilivyokuwa kwa baba zake, bali kwa misingi ya uwezo wa uzima usioharibika.

Tazama sura Nakili




Waebrania 7:16
15 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni, bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.


Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia.


Bali sasa, mkiisha kumjua Mungu, ya nini kurejea tena kwa mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge na yenye upungufu ambayo mnataka kuyatumikia tena.


akiisba kuifuta ile khati iliyoandikwa na kutushitaki kwa hukumu zake; iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwe kati kati yetu sisi na yeye, akaikaza msalabani;


Bassi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkaacha mafundisho ya awali ya ulimwengu, ya nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,


BASSI kwa kuwa torati ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo, kwa dhahihu zile zile wanazozitoa killa mwaka daima, hawawezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.


Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine kwa mfano wa Melkizedeki;


maana ashuhudu, kwamba, Wewe u kuliani hatta milele kwa daraja la Melkizedeki.


(maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; hali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe kuhani hatta milele kwa daraja la Melkizedeki;)


Maana torati yawaweka wana Adamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka Mwana, aliyekamilika hatta milele.


hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhayi wake, bali amefanauishwa na Mwaua wa Mungu,) adumu kuhani milele.


bassi si zaidi damu yake Kristo, ambae kwamba kwa Roho ya milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo mawaa, itawasafisheni dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hayi?


na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo