Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 7:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lolote la kuikhusu katika mambo ya ukuhani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Inafahamika wazi kwamba yeye alizaliwa katika kabila la Yuda ambalo Mose hakulitaja alipokuwa anasema juu ya makuhani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Inafahamika wazi kwamba yeye alizaliwa katika kabila la Yuda ambalo Mose hakulitaja alipokuwa anasema juu ya makuhani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Inafahamika wazi kwamba yeye alizaliwa katika kabila la Yuda ambalo Mose hakulitaja alipokuwa anasema juu ya makuhani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda, tena kuhusu kabila hilo Musa hakusema lolote kwa habari za makuhani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kwa maana ni dhahiri kwamba Isa Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda, tena kuhusu kabila hilo Musa hakusema lolote kwa habari za makuhani.

Tazama sura Nakili




Waebrania 7:14
22 Marejeleo ya Msalaba  

Na wewe Bethlehemu wa inchi ya Yuda, Huwi mdogo kamwe katika majumbe ya Yuda: Kwa kuwa kwako atatoka liwali Atakaewachunga watu wangu Israeli.


Na latoka wapi neno hili lililonipata, mama wa Bwana wangu anijilie mimi?


wa Aminadab, wa Aram, wa Esrom, wa Fares, wa Yuda,


Nao wakamwambia, Bibi, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala sijui walikomweka.


Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu, na Mungu wangu.


khabari za Mwana wake, aliyekuwa katika ukoo wa Daud kwa jinsi ya mwili,


Ee bin-Adamu, uwahukumuye wale wafanyao hayo na kutenda yayo hayo mwenyewe, je! wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu?


Atukuzwe Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani ya Kristo;


Naam, naliona mambo yote kuwa khasara kwa ajili ya uzuri usio kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambae kwa ajili yake nimepata khasara ya mambo yote, nikiyahesabu kuwa kania mavi illi nimpate Kristo;


Maana yeye aliyenenwa hayo alikuwa mshirika wa kahila nyingine, wala hapana mtu wa kahila hii aliyeikhudumia madhbahu.


Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine kwa mfano wa Melkizedeki;


Mimi Yesu nalimtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daud, ile nyota yenye kungʼaa ya assubuhi.


Na mmoja wa wale wazee akaniambia, Usilie, tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, shina la Daud, yeye amepata uwezo wa kukifunua kitabu na kuzivunja zile muhuri saba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo