Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waebrania 7:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Bassi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi: (maana watu wale waliipata sharia kwa huo) kulikuwa na haja gani tena kuhani mwingine aondoke, wa daraja la Melkizedeki, wala si kwa daraja la Haruni?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Kutokana na ukuhani wa Walawi, watu wa Israeli walipewa sheria. Sasa, kama huduma ya Walawi ingalikuwa kamilifu, hapangekuwa tena na haja ya kutokea ukuhani mwingine tofauti, na ambao umefuata utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki, na si ule wa Aroni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Kutokana na ukuhani wa Walawi, watu wa Israeli walipewa sheria. Sasa, kama huduma ya Walawi ingalikuwa kamilifu, hapangekuwa tena na haja ya kutokea ukuhani mwingine tofauti, na ambao umefuata utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki, na si ule wa Aroni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Kama ukamilifu ungeweza kupatikana kupitia kwa ukuhani wa Walawi (kwa kuwa katika msingi huo, sheria ilitolewa kwa watu), kwa nini basi kulikuwa na haja ya kuja kuhani mwingine: kuhani kwa mfano wa Melkizedeki, wala si kwa mfano wa Haruni?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Kama ukamilifu ungeweza kupatikana kwa njia ya ukuhani wa Walawi (kwa kuwa katika msingi huo, sheria ilitolewa kwa watu), kwa nini basi imekuwepo haja ya kuja kuhani mwingine: kuhani kwa mfano wa Melkizedeki, wala si kwa mfano wa Haruni?

Tazama sura Nakili

Waebrania 7:11
17 Marejeleo ya Msalaba  

Siibatili neema ya Munga. Maana, ikiwa haki hupatikana kwa sharia, bassi, Kristo alikufa burre.

Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia.

Bali sasa, mkiisha kumjua Mungu, ya nini kurejea tena kwa mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge na yenye upungufu ambayo mnataka kuyatumikia tena.

ametajwa na Mungu kuwa Kuhani mkuu kwa mfano wa daraja la Melkizedeki.

kama asemavyo mahali pengine, Wewe u Kuhani milele Kwa mfano wa daraja la Melkizedeki.

alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa Kuhani mkuu kwa jinsi ya Melkizedeki hatta milele.

kwa maana alikuwa katika viuno vya bada yake Ibrahimu, hapo Melkizedeki alipokutana nae.

Maana ukuhani ule ukihadilika, hapana buddi sharia nayo ibadilike.

Maana yeye aliyenenwa hayo alikuwa mshirika wa kahila nyingine, wala hapana mtu wa kahila hii aliyeikhudumia madhbahu.

Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine kwa mfano wa Melkizedeki;

(maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; hali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe kuhani hatta milele kwa daraja la Melkizedeki;)

Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili.

Bassi, vitu hivi vikiislia kutengenezwa hivyo, makuhani huingia khema ya kwanza siku zote, wakiyatimiza mambo va ibada.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo