Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 6:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Maana watu waliokwisha kuangaziwa, wakaonja zawadi za mbinguni, wakashirikishwa Roho Mtakatifu

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Maana watu waliokwisha kuangaziwa, wakaonja zawadi za mbinguni, wakashirikishwa Roho Mtakatifu

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Maana watu waliokwisha kuangaziwa, wakaonja zawadi za mbinguni, wakashirikishwa Roho Mtakatifu

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Kwa kuwa ni vigumu kwa wale ambao wakati fulani walishapata nuru, ambao walishaonja kipawa cha mbinguni, ambao wamekwisha kushiriki katika Roho wa Mungu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Kwa kuwa ni vigumu kwa wale ambao wakati fulani walishapata nuru, ambao walishaonja kipawa cha mbinguni, ambao wamekwisha kushiriki katika Roho wa Mwenyezi Mungu,

Tazama sura Nakili




Waebrania 6:4
38 Marejeleo ya Msalaba  

Marra huenda, akachukua pamoja nae pepo wengine saba walio waovu kupita nafsi yake, nao huingia na kukaa humo; na mambo, ya mwisho ya mtu yule huwa mabaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kiovu.


Ninyi ni chumvi ya dunia: lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwani ikolee? Haifai tena kabisa, illa kufupwa nje na kukanyagwa na watu.


Mtu asipokaa ndani yangu, atupwa nje kama tawi, akauka; huyakusanya, huyatupa motoni, yakateketea.


Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni.


Yesu akajibu akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, nae ni nani akuambiae, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, nae angalikupa maji yaliyo hayi.


Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa mkate ule kutoka mbinguni, bali Baba yangu anawapa mkate ule utokao mbinguni ulio wa kweli.


Na wale waliotahiriwa walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu mataifa nao wameshukiwa kipaji cha Roho Mtakatifu.


Bassi ikiwa Mwenyiezi Mungu amewapa wao karama ile ile aliyotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani niweze kumpinga Mungu?


Na Mungu, ajuae mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vilevile kama alivyotupa sisi;


Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhani ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.


kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapeni karama ya rohoni, illi mfanywe imara;


ambao mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.


Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itangʼaa toka gizani, ndive aliyengʼaa mioyoni mwetu, atupe nuru va elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.


Nataka kujifunza neno bili moja kwenu. Mlipokea Roho kwa matendo ya sharia, au kwa kusikia kunakotokana na imani?


Bassi, yeye awaruzukiae Roho na kufanya miujiza kati yenu, afanya hayo kwa matendo ya sharia, au kwa kusikia kunakotokana na imani?


macho ya akili zenu yakitiwa nuru, mjue tumaini la wito wake jinsi lilivyo, na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo,


Maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu:


ambayo nilifanywa mkhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema yake Mungu niliyopewa kwa kadiri ya kutenda kazi kwa uweza wake.


Lakini killa mmoja wetu alipewa neema, kwa kadiri ya kipawa cha Kristo.


Usiache kuitumia ile karama iliyo udani yako uliyopewa wewe kwa unabii, na kwa kuwekewa mikono ya wazee.


akiwaonya kwai npole washindanao nae, illi, kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na ujuzi wa kweli,


Iskander mfua shaba alinionya mabaya mengi; Bwana atamlipa kwa jinsi ya matendo yake.


Lakini zikumbukeni siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu;


Mungu nae akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.


Mtu akimwona ndugu yake anakosa kosa lisilo la mauti, ataomba, nae atampa uzima kwa ajili ya hawo wakosao kosa lisilo la mauti. Liko kosa lililo la mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hilo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo