Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 6:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa Kuhani mkuu kwa jinsi ya Melkizedeki hatta milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Yesu mwenyewe ametangulia kuingia humo kwa ajili yetu na amekuwa kuhani mkuu milele, kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Yesu mwenyewe ametangulia kuingia humo kwa ajili yetu na amekuwa kuhani mkuu milele, kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Yesu mwenyewe ametangulia kuingia humo kwa ajili yetu na amekuwa kuhani mkuu milele, kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 ambapo Isa mtangulizi wetu aliingia kwa niaba yetu. Yeye amekuwa Kuhani Mkuu milele, kwa mfano wa Melkizedeki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 mahali ambapo Isa mtangulizi wetu aliingia kwa niaba yetu. Yeye amekuwa Kuhani Mkuu milele, kwa mfano wa Melkizedeki.

Tazama sura Nakili




Waebrania 6:20
20 Marejeleo ya Msalaba  

Ni nani atakaewahukumu? Kristo ndiye aliyekufa, naam, na zaidi ya haya, amefufuka, nae yuko mkono wa kuume wa Mungu, tena ndiye anaetuombea.


Atukuzwe Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani ya Kristo;


Yeye kwa kuwa ni mwanga wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivitengeneza vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya peke yake utakaso wa dhambi zetu, aliketi juu mkono wa kuume wa ukuu;


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


Kwa kuwa ilimpasa veye, ambae kwa ajili yake na kwa kazi yake vitu vyote vimekuwa, akileta wana wengi hatta utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokofu wao kwa mateso.


Kwa hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, illi afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.


KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,


Bassi, iwapo tunae kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, tujashike sana maungamo yetu.


ametajwa na Mungu kuwa Kuhani mkuu kwa mfano wa daraja la Melkizedeki.


kama asemavyo mahali pengine, Wewe u Kuhani milele Kwa mfano wa daraja la Melkizedeki.


BASSI, katika hayo tuuayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunae kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu mbinguni,


wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia marra moja katika patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.


Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyiku kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu palipo patakatifu khalisi; hali aliingia mbinguni khassa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;


alioko mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zimetiishwa chini yake.


Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo