Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 6:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 maana Mungu si dhalimu hatta asahau kazi zenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewakhudumia watakatifu, na hatta hivi sasa mngali mkiwakhudumia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo mliyoonesha kwa ajili yake katika huduma mliyowapa na mnayowapa sasa watu wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo mliyoonesha kwa ajili yake katika huduma mliyowapa na mnayowapa sasa watu wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Mungu hakosi haki; yeye hataisahau kazi mliyoifanya au upendo mliyoonesha kwa ajili yake katika huduma mliyowapa na mnayowapa sasa watu wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Mungu si mdhalimu: yeye hataisahau kazi yenu na upendo ule mlioonesha kwa ajili yake katika kuwahudumia watakatifu na hata sasa mnaendelea kuwahudumia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Mwenyezi Mungu si mdhalimu: yeye hataisahau kazi yenu na upendo ule mlioonyesha kwa ajili yake katika kuwahudumia watakatifu na hata sasa mnaendelea kuwahudumia.

Tazama sura Nakili




Waebrania 6:10
48 Marejeleo ya Msalaba  

Na mtu aliye yote atakaemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa kikombe cha maji ya baridi tu, kwa kuwa yu mwanafunzi, amin, nawaambieni, haitampotea kamwe thawabu yake.


Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, Enendeni na ninyi katika shamba la mizabibu, na iliyo haki mtapata.


Vilevile na yule mwenye mbili, yeye nae akachuma nyingine mbili faida.


Kwa kuwa ye yote atakaewanywesha ninyi kikombe cha maji kwa jina langu, kwa kuwa ninyi watu wa Kristo, amin nawaambieni hatakosa thawabu yake.


Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeae ye yote nimpelekae, anipokea mimi; nae anipokeae mimi, ampokea yeye aliyenipeleka.


Kornelio, maombi yako yamesikiwa, na sadaka zako zinakumbukwa mbele za Mungu.


Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Maombi yako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.


Na wale wanafunzi, killa mtu kwa kadiri alivyofanikiwa wakaazimu kupeleka msaada kwa ndugu zao waliokaa Yahudi.


kwa mahitaji ya watakatifu, mkiwashirikisha; katika kukaribisha wageni, mkijitahidi.


KWA khabari za kuwakhudumia watakatifu sina haja ya kuwaandikia.


Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali khudumianeni kwa upendo.


Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.


Tuwapo na nafasi na tuwatendee watu wote mema; khassa watu walio wa nyumba ya imani.


Na killa mfanjalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.


wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya amani, na taabu yenu ya upendo, na uvumilivu wenu wa tumaini lililo katika Bwana Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu;


watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo,


baada ya haya nimewekewa taji ya baki, ambayo Bwana mhukumu wa haki atanipa katika siku ile: wala si mimi tu, bali watu wote pia waliopenda kutokea kwake.


Lakini zikumbukeni siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu;


Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana na watu; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.


Tukiziungama dhambi zetu, yu amini na wa haki atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha udhalimu wote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo