Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 6:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 KWA sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo illi tuuflkilie utimilifu; tusiweke misingi tena, yaani kuzitubia kazi zisizo na uhayi, na kuwa na imani kwa Mungu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Basi, tuyaache nyuma yale mafundisho ya mwanzomwanzo juu ya Kristo, tusonge mbele kwa yale yaliyokomaa, na sio kuendelea kuweka msingi kuhusu kuachana na matendo ya kifo, na juu ya kumwamini Mungu;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Basi, tuyaache nyuma yale mafundisho ya mwanzomwanzo juu ya Kristo, tusonge mbele kwa yale yaliyokomaa, na sio kuendelea kuweka msingi kuhusu kuachana na matendo ya kifo, na juu ya kumwamini Mungu;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Basi, tuyaache nyuma yale mafundisho ya mwanzomwanzo juu ya Kristo, tusonge mbele kwa yale yaliyokomaa, na sio kuendelea kuweka msingi kuhusu kuachana na matendo ya kifo, na juu ya kumwamini Mungu;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Kwa hiyo, tukiachana na mafundisho yale ya awali kuhusu Al-Masihi na tukisonga mbele ili tufikie utimilifu, tusiweke tena msingi wa mafundisho ya kuzitubia kazi zisizo na uhai na imani katika Mungu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kwa hiyo, tukiachana na mafundisho yale ya awali kuhusu Al-Masihi na tukisonga mbele ili tufikie utimilifu, sio kuweka tena msingi wa mafundisho ya kuzitubia kazi zisizo na uhai na imani katika Mwenyezi Mungu,

Tazama sura Nakili




Waebrania 6:1
50 Marejeleo ya Msalaba  

Akajibu akasema, Sitaki; baadae akatubu, akaenda.


Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, nanyi hamkumwamini; lakini watoza ushuru na makahaha walimwamini: nanyi mlipoona, hamkutuhu haada ya haya, na kumwamini.


Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


Tokea wakati huo Yesu akaanza kukhubiri, na kusema, Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


Bassi mwe ninyi wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.


mvua ikanya, maji mengi yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa katika mwamba.


Mwanzo wa injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu;


Wakatoka, wakakhubiri kwamba watu watubu.


Mfano wake ni mtu ajengae nyumba, akafukua, akachimba chini sana, akaweka msingi wake juu ya mwamba. Bassi palipokuwa na gharika, mto ukairukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa, kwa kuwa msingi wake umewekwa juu ya mwamba.


Yesu akapaaza sauti yake akasema, Aniaminiye mimi, haniamini mimi, bali yeye aliyenipeleka.


MSIFADHAIKE mioyo yenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.


Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima.


Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Bassi, Mungu amewajalia mataifa nao toba liletalo uzima.


Bassi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hauoni; bali sasa anawakhuhiri watu wote wa killa mahali watubu.


Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe killa mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.


nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani toba iliyo kwa Mungu, na imani iliyo kwa Bwana wetu Yesu Kristo.


hali kwanza niliwakhubiri wale wa Dameski na Yerusalemi, na katika inchi yote ya Yahudi, na watu wa mataifa, watubu wakamwelekee Mungu, wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao.


Tubuni bassi, mrejee, illi dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuhurudishwa kwa kuwako kwake Bwana:


lakini ijapo iliyo kamili, iliyo kwa, sehemu itabatilika.


Illakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; nayo si hekima ya dunia hii, wala yao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilishwa;


BASSI, kwa kuwa tuna ahadi hizo, wapenzi, tujitakase nafsi zelu uchafu wote wa mwili na roho, tukitimiza utakatifu katika kumeha Mungu.


Maana huzuni iliyo mbele za Mungu hufanyiza toba iletayo wokofu isiyo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanyiza mauti.


NA ninyi, mlipokmva wafu kwa sababu ya makosa yenu na dhambi zemi,


hatta wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu, alituhuisha pamoja na Kristo (mmeokolewa kwa neema);


kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, kazi ya khuduma itendeke, mwili wa Kristo ujengwe;


ambae sisi tunakhubiri khabari zake, tukimwonya killa mtu, na tukimfundisha killa mtu katika hekima yote, tupate kumleta killa mtu mtimilifu katika Kristo Yesu;


Juu ya haya yote vaeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.


Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu, katika maombi yake msimame wakamilifu mkathuhutike sana katika mapenzi yote ya Mungu.


Na bila shaka siri ya utawa ni kuu. Mungu alidhibirishwa katika mwili, alihesabiwa kuwa na wema katika roho, alionekana na malaika, alikhubiriwa katika mataifa, aliaminiwa katika ulimwengu, alichukuliwa juu katika utukufu.


wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao illi wapate uzima wa milele.


Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake; tena, killa alilajae jina la Bwana na aache uovu.


Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu ampendezae Mungu lazima aamini kwamba yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.


mkaifanyia miguu yenu njia za kunyoka, illi kitu kilicho kilema kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.


Bassi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi: (maana watu wale waliipata sharia kwa huo) kulikuwa na haja gani tena kuhani mwingine aondoke, wa daraja la Melkizedeki, wala si kwa daraja la Haruni?


bassi si zaidi damu yake Kristo, ambae kwamba kwa Roho ya milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo mawaa, itawasafisheni dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hayi?


Na saburi iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa neno.


ambae kwa yeye mlimwamini Mungu, aliyemfufua akampa utukufu; hatta imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo limekamilishwa ndani yetu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo