Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 5:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 nae alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokofu wa milele kwa watu wote wanaomtii;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Na alipofanywa mkamilifu, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Na alipofanywa mkamilifu, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Na alipofanywa mkamilifu, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 naye akiisha kukamilishwa, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 na akiisha kukamilishwa, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii.

Tazama sura Nakili




Waebrania 5:9
39 Marejeleo ya Msalaba  

Alipokuwa akisema, wingu jeupe likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, niliyependezwa nae; msikieni yeye.


Akawaambia, Enendeni zenu, nikamwambie yule mbweha, Tazama, nafukuza pepo, nafanya kazi ya kuwaponya watu leo na kesho, nami siku ya tatu nakamilika.


Bassi Yesu alipoipokea siki, akasema, Imekwisha: akainama kichwa, akatoa roho.


mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambae Mungu amemfufua: na sisi tu mashahidi wake.


Wala hakuna wokofu katika mwingine aliye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wana Adamu litupasalo kuokolewa nalo.


Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambae Mungu amewapa wote wamtiio.


ambae katika yeye tulipokea neema na utume illi mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake;


Lakini si wote walioitii khahari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, nani aliyeamini khabari zetu?


Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yanga, mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo, kwa nguvu za ishara na maajabu,


na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, hasira na ghadhabu;


Lakini Mungu ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;


tukiangusha mawazo na kiila kitu kilichoinuka, kijiinuacho jun ya elimu ya Mungu; na tukifanya mateka fikara zote zipate kumtii Kristo:


Bassi, wapendwa, kama vile mlivyotii siku zote, si wakati mimi nilipokuwapo, bali sasa zaidi mimi nisipokuwapo, utimizeni wokofu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka;


katika mwako wa moto, akiwalipa kisasi wao wasiomjua Mungu, nao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo;


Na Bwana wetu Yesu Kristo, na Mungu Baba yetu aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema,


Kwa ajili ya hilo nastahimili yote, kwa ajili ya wateule, wao nao waupate wokofu ulio katika Kristo Yesu pamoja ua utukufu wa milele.


Hawo wote si roho zitumikazo, wakitumwa kuwakhudumu wale watakaourithi wokofu?


kwa kuwa Mungu ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, illi wasikamilishwe pasipo sisi.


Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, akatoka aende hatta mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


Kwa kuwa ilimpasa veye, ambae kwa ajili yake na kwa kazi yake vitu vyote vimekuwa, akileta wana wengi hatta utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokofu wao kwa mateso.


sisi je! tutapataje kujiponya, tusipotunza wokofu mkiju namna hii? ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kiisha nkathubutika kwetu na wale waliosikia;


wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia marra moja katika patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.


Na kwa sababu hii yu mjumbe wa agauo jipya, illi, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa ya katika agano la kwanza, walioitiwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.


kadhalika Kristo, akiisha kutolewa sadaka marra moja aziondoe dhambi za watu wengi, marra ya pili, pasipo dhambi, ataonekana nao wamtazamiao kwa wokofu.


Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;


Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele.


jilindeni katika upendo wa Mungu, mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Krislo, hatta mpate uzima wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo