Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 5:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Yeye siku hizo za niwili wake alimtolea yeye awezae kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa sababu ya kicho chake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Yesu alipokuwa anaishi hapa duniani, kwa kilio kikuu na machozi, alisali na kumwomba Mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kumwokoa kifoni; naye alisikilizwa kwa sababu ya kumcha Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Yesu alipokuwa anaishi hapa duniani, kwa kilio kikuu na machozi, alisali na kumwomba Mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kumwokoa kifoni; naye alisikilizwa kwa sababu ya kumcha Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Yesu alipokuwa anaishi hapa duniani, kwa kilio kikuu na machozi, alisali na kumwomba Mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kumwokoa kifoni; naye alisikilizwa kwa sababu ya kumcha Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Katika siku za maisha ya Isa hapa duniani, alimtolea maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, yeye awezaye kumwokoa na mauti, naye Mungu akamsikia kwa sababu ya kutii kwake kwa unyenyekevu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Katika siku za maisha ya Isa hapa duniani, alimtolea maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, yeye awezaye kumwokoa na mauti, naye Mwenyezi Mungu akamsikia kwa sababu ya kutii kwake kwa unyenyekevu.

Tazama sura Nakili




Waebrania 5:7
38 Marejeleo ya Msalaba  

Na kama saa tissa, Yesu akapaaza sauti yake kwa nguvu akinena, Eli, Eli, lama sabakhthani? maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?


Nae Yesu akiisha kupaaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.


Na saa tissa Yesu akapiga kelele kwa sauti kuu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? tafsiri yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?


Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho.


Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu: na alipokwisha kusema haya akatoa roho.


Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.


Yesu akatoka machozi.


Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya makutano hawa wanaozunguka nalisema haya, wapate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma.


MANENO hayo aliyasema Yesu: akainua macho yake kuelekea mbinguni, akanena, Baba, saa ile imekuja. Mtukuze Mwana wako, illi Mwana wako nae akutukuze wewe;


Maana yale yasiyowezekana kwa sharia, kwa kuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa ajili ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili:


Hatta ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwana wake, amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sharia,


Na bila shaka siri ya utawa ni kuu. Mungu alidhibirishwa katika mwili, alihesabiwa kuwa na wema katika roho, alionekana na malaika, alikhubiriwa katika mataifa, aliaminiwa katika ulimwengu, alichukuliwa juu katika utukufu.


Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo marra moja.


Kwa biyo ajapo ulimwenguni, anena, Dhambi na toleo hukutaka, lakini mwili uliniwekea tayari:


Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu khabari za mambo yasiyoonekana bado, kwa kumcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Kwa hiyo akauhukumu ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.


Bassi tukipokea ufalme usioweza kutetemeshwa, tuwe na neema, illi kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho:


Bassi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka wafu Mchungaji wa kondoo aliye mkuu, kwa damu ya agano la milele, Bwana wetu Yesu,


Bassi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye nae vivyo hivyo alishiriki yayo bayo, illi kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani Shetani,


Na killa roho isiyoungama kwamba Yesu Kristo amekujii katika mwili, haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya adui wa Kristo ambae mmesikia kwamba yuaja; na sasa amekwisha kuwamo duniani.


Kwa maana wadanganyifu wengi wameingia katika dunia, wasio-ungama ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na adui wa Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo