Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 4:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Bassi, iwapo tunae kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, tujashike sana maungamo yetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Basi, tuzingatie kwa makini imani tunayoiungama. Maana tunaye Kuhani Mkuu aliyeingia mpaka mbinguni; Yesu, Mwana wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Basi, tuzingatie kwa makini imani tunayoiungama. Maana tunaye Kuhani Mkuu aliyeingia mpaka mbinguni; Yesu, Mwana wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Basi, tuzingatie kwa makini imani tunayoiungama. Maana tunaye Kuhani Mkuu aliyeingia mpaka mbinguni; Yesu, Mwana wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kwa kuwa tunaye Kuhani Mkuu kuliko wote ambaye ameingia mbinguni, Isa Mwana wa Mungu, basi na tushikamane sana kwa uthabiti na ule ukiri wa imani yetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kwa kuwa tunaye Kuhani Mkuu kuliko wote ambaye ameingia mbinguni, Isa Mwana wa Mwenyezi Mungu, basi na tushikamane sana kwa uthabiti na ule ukiri wa imani yetu.

Tazama sura Nakili




Waebrania 4:14
31 Marejeleo ya Msalaba  

Mjaribu akamjia akasema, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.


Mwanzo wa injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu;


Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.


Ikawa katika kuwabariki, akajitenga nao, akachukuliwa juu mbinguni.


wakasema, Watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.


ambae ilimpasa kupokewa mbinguni hatta zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa vinywa vya manabii wake tokea mwanzo wa ulimwengu.


Ni nani atakaewahukumu? Kristo ndiye aliyekufa, naam, na zaidi ya haya, amefufuka, nae yuko mkono wa kuume wa Mungu, tena ndiye anaetuombea.


Namjua mtu mmoja katika Kristo, impita sasa miaka arobatashara, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui, Mungu ajua). Mtu huyu alichukuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.


kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huu, mnamtukuza Mungu kwa ajili ya ntii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote.


Aliyeshuka ndiye aliyepanda juu sana kupita mbingu zote, vitu vyote vijae nae.)


Lakini katika khabari ya Mwana anena, Kiti chako, Mungu, ni cha milele; na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya kunyoka.


Lakini huyu, alipokwisha kutoa dhabihu nioja kwa dhambi, idumuyo hatta milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu;


Tulishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni amini;


Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa nayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho ya neema?


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


KWA hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi yaliyasikiwa tusije tukayakosa.


Kwa hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, illi afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.


KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,


Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu mpaka mwisho;


alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa Kuhani mkuu kwa jinsi ya Melkizedeki hatta milele.


wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hatta wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu marra ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.


hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhayi wake, bali amefanauishwa na Mwaua wa Mungu,) adumu kuhani milele.


BASSI, katika hayo tuuayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunae kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu mbinguni,


wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia marra moja katika patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.


Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyiku kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu palipo patakatifu khalisi; hali aliingia mbinguni khassa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;


alioko mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zimetiishwa chini yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo