Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 4:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Maana Neno la Mungu li hayi, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko ukali wa upanga ukatao kuwili, tena lachoma kiasi cha kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Neno la Mungu ni hai na lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili. Hukata kabisa mpaka mahali ambapo moyo na roho hukutana, mpaka pale vikutanapo viungo vya mwili na uboho. Neno hilo huchambua nia na fikira za mioyo ya watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Neno la Mungu ni hai na lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili. Hukata kabisa mpaka mahali ambapo moyo na roho hukutana, mpaka pale vikutanapo viungo vya mwili na uboho. Neno hilo huchambua nia na fikira za mioyo ya watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Neno la Mungu ni hai na lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili. Hukata kabisa mpaka mahali ambapo moyo na roho hukutana, mpaka pale vikutanapo viungo vya mwili na uboho. Neno hilo huchambua nia na fikira za mioyo ya watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kwa maana neno la Mungu li hai tena lina nguvu. Lina makali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili, hivyo linachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, viungo na mafuta yaliyo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kwa maana Neno la Mwenyezi Mungu li hai tena lina nguvu. Lina makali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili, hivyo linachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, viungo na mafuta yaliyo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

Tazama sura Nakili




Waebrania 4:12
42 Marejeleo ya Msalaba  

Na mfano ndio huu: Mbegu ni neno la Mungu.


Anikataae mimi, asiyekubali maneno yangu, anae amhukumuye: neno lile nililolisema, ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.


Mimi ni mkate wa uzima ulioshuka kutoka mbinguni; mtu akila mkate huu, ataishi milele: na mkate nitakaotoa mimi ni nyama yangu nitakayotoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.


Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?


Hatta walipokwisha kumwomba Mungu, pahali paie walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa uthabiti.


Waliposikia wakachomwa mioyo yao; wakafanya shauri kuwaua.


Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema nae katika mlima Sinai, tena pamoja na baba zetu: ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi.


kwa maana siionci haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokofu, kwa killa aaminiye, kwa Myahudi kwanza, hatta kwa Myunani pia.


bali kwao waitwao, Wayahudi na Wayunani pia, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.


Kwa maana sisi si kama wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama watu wasemao kwa weupe wa moyo, kaina watu watumwao na Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.


lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyosetirika, wala hatuenendi kwa ujanja, wala kulichanganya neno la Mungu na uwongo; hali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mhele za Mungu.


Lakini yote yakemewapo, hudhihirishwa na nuru; maana killa kitu kinachodhihirisha ni nuru.


kusudi alitakase na kulisafisha kwa maji, na kwa Neno;


Tena ipokeeni chepeo ya wokofu, na upanga wa Roho, ndio neno la Mungu;


Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa mlipopokea lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la kibinadamu; bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli, litendalo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.


Mungu wa amani mwenyewe awatakase kahisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.


Wakumbukeni wale waliokuwa na mamlaka juu yenu, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa maisha zao, iigeni imani yao.


na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,


Alipopenda alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limhuko la viumbe vyake.


kwa kuwa mmezaliwa marra ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, bali isiyoharibika, kwa neno la Mungu lenye uzima, na lidumulo hatta milele.


Nae alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume: na upanga mkali, mkali kuwili, watoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua likingʼaa kwa nguvu zake.


Na upanga mkali hutoka kinywani mwake awapige mataifa kwa huo. Nae atawachunga kwa fimbo ya chuma, nae anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ukali wa ghadhabu ya Mungu Mwenyiezi.


na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya farasi yule, utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.


Tubu; na usipotubu naja kwako upesi, nitafanya vita juu yako kwa upanga wa kinywa changu.


nami nitawaua watoto wake kwa manti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzae viuno na mioyo. Nami nitampa killa mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yenu.


Nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, wakapewa hukumu: nikaona roho zao waliokatwa kichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia nyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea alama yake katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; wakawa hayi, wakamiliki pamoja na Kristo miaka elfu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo