Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 3:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Na Musa alikuwa mwaminifu katika nyumba yake yote kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Mose alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Bwana kama mtumishi, na alinena juu ya mambo ambayo Mungu atayasema hapo baadaye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Mose alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Bwana kama mtumishi, na alinena juu ya mambo ambayo Mungu atayasema hapo baadaye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Mose alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Bwana kama mtumishi, na alinena juu ya mambo ambayo Mungu atayasema hapo baadaye.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Musa, kama mtumishi, alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu, akishuhudia kwa yale Mungu angeyasema baadaye.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Basi Musa kama mtumishi alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu, akishuhudia kwa yale ambayo yangetamkwa baadaye.

Tazama sura Nakili




Waebrania 3:5
35 Marejeleo ya Msalaba  

Nani bassi aliye mtumishi yule amini mwenye haki, ambae bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape chakula kwa saa yake?


Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema, na amini: ulikuwa amini kwa machache, nitakuweka juu ya mengi: ingia katika furaha ya bwana wako.


Bwana akasema, Nani, bassi, aliye wakili mwaminifu niwenye busara, ambae Bwana wake atamweka juu ya ntumishi wake wote, awape watu posho lao kwa saa yake?


Akaanza toka Musa na manabii, akawafasiria katika maandiko yote mambo yaliyomkhusu yeye.


Akawaambia, Haya ndiyo maneno yangu niliyowaambieni, nilipokuwa kwenu, ya kuwa hayana buddi kutimizwa yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii, na katika zaburi.


Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake: na hayo ndiyo yanayonishuhudia:


Wakiislia kuwekana kwa siku, wakaja kwake nyumbani kwake, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sharia ya Musa na ya manabii, tangu assubuhi hatta jioni.


Musa huyo ndiye aliyewaambia wana wa Israeli, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii katika ndugu zenu, kama mimi: mtamsikia huyo.


Sasa, lakini, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sharia, inashuhudiwa na torati na manabii,


Tena inayohitajiwa katika mawakili, ndio mtu aonekane amini.


Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu aliyenitia nguvu, kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akiniweka katika khuduma yake;


KWA sehemu nyingi na kwa namna nyingi Mungu zamani alisema na babu zetu katika manabii,


Yesu, aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemfanya, kama Musa nae alivyokuwa katika nyumba yake yote.


Maana killa nyumba imetengenezwa na mtu; illa yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu.


watumikao kwa mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile khema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.


Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyiku kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu palipo patakatifu khalisi; hali aliingia mbinguni khassa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;


Nao wauimba uimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na uimbo wa Mwana kondoo, wakisema, Makuu, ya ajabu, matendo yako, ee Bwana Mungu Mwenyiezi; za haki, za kweli njia zako, ee Mfalme wa watakatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo