Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 2:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 illa twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, illi kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya killa mtu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Lakini twamwona Yesu ambaye alifanywa kwa kitambo kidogo kuwa chini kuliko malaika, ili kwa neema ya Mungu afe kwa ajili ya watu wote. Sasa tunamwona ametawazwa kwa utukufu na heshima kwa sababu ya kifo alichoteseka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Lakini twamwona Yesu ambaye alifanywa kwa kitambo kidogo kuwa chini kuliko malaika, ili kwa neema ya Mungu afe kwa ajili ya watu wote. Sasa tunamwona ametawazwa kwa utukufu na heshima kwa sababu ya kifo alichoteseka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Lakini twamwona Yesu ambaye alifanywa kwa kitambo kidogo kuwa chini kuliko malaika, ili kwa neema ya Mungu afe kwa ajili ya watu wote. Sasa tunamwona ametawazwa kwa utukufu na heshima kwa sababu ya kifo alichoteseka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Lakini twamwona Isa, aliyefanywa chini kidogo kuliko malaika, sasa akiwa amevikwa taji la utukufu na heshima kwa sababu alistahimili mauti, ili kwa neema ya Mungu apate kuonja mauti kwa ajili ya kila mtu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Lakini twamwona Isa, aliyefanywa chini kidogo kuliko malaika, sasa akiwa amevikwa taji ya utukufu na heshima kwa sababu alistahimili mauti, ili kwamba kwa neema ya Mwenyezi Mungu apate kuonja mauti kwa ajili ya kila mtu.

Tazama sura Nakili




Waebrania 2:9
39 Marejeleo ya Msalaba  

Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawo wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hatta watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.


Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini khabari za maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayatendi kazi, wala hayasokoti:


AKAWAAMBIA, Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa ambao hawataonja mauti hatta watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu.


Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataionja mauti kabisa hatta watakapouona ufalme wa Mungu.


Siku ya pili yake Yohana amwona Yesu anakuja kwake, akanena, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuae dhambi ya ulimwengu!


Ndio maana Baba anipenda, kwa sababu nauweka uzima wangu illi niutwae tena.


Nami nikiinuliwa juu ya inchi nitavuta wote kwangu.


Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hatta akampeleka Mwana wake wa pekee, illi mtu aliye yote amwaminiye asipotee, bali apate uzima wa milele.


Amin, amin, nawaambieni, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti kabisa hatta milele.


Bassi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumefahamu ya kuwa una pepo; Ibrahimu amekufa na manabii, na wewe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti kabisa hatta milele.


Bassi akiisha kupandishwa hatta mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.


Mungu wa Ibrahimu na Isaak na Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambae ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe.


Bassi tena, kama vile kwa anguko moja watu wote walihukumiwa, vivyo hivyo kwa tendo moja la haki watu wote walipewa haki yenye uzima.


Bali Mungu aonyesha pendo lake kwetu, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.


Maana yale yasiyowezekana kwa sharia, kwa kuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa ajili ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili:


Yeye asiyemwachilia Mwana wake yeye, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukarimia na vitu vyote pamoja nae?


tena alikufa kwa ajili ya wote, illi walio hayi wasiwe hayi kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.


Maana alimfanya yeye asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili vefu, illi sisi tuwe haki ya Mungu katika Yeye.


Hatta ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwana wake, amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sharia,


aliyejitoa nafsi yake kuwa ukombozi kwa ajili ya wote utakaoshuhudiwa kwa majira yake;


Umependa haki, umechukia maasi: kwa sababu hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, mafuta ya shangwe kupita wenzako.


Kwa biyo ajapo ulimwenguni, anena, Dhambi na toleo hukutaka, lakini mwili uliniwekea tayari:


Kwa imani Enok alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha: maana kabla ya kuhamishwa kwake alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


Umemfanya mdogo punde kuliko malaika, umemvika taji ya utukufu na heshima, umemweka jua ya kazi za mikono yako;


Nae, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye; maana yu hayi siku zote illi awaombee.


Maana killa kuhani mkuu awekwa illi atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu nae awe na kitu akitoe.


ambae kwa yeye mlimwamini Mungu, aliyemfufua akampa utukufu; hatta imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.


nae ni kipatanisho kwa dhambi zetu: wala si kwa dhambi zetu tu, bali kwa dhambi za ulimwengu wote.


Na macho yake yalikuwa kama mwako wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi, nae ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu illa yeye mwenyewe.


Nao waimba uimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulicbinjwa


Tufuate:

Matangazo


Matangazo