Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 2:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Kwa hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, illi afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Ndiyo maana ilimbidi awe kama ndugu zake kwa kila namna, ili awe Kuhani Mkuu wao aliye mwaminifu na mwenye huruma katika kumtumikia Mungu, ili dhambi za watu ziondolewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Ndiyo maana ilimbidi awe kama ndugu zake kwa kila namna, ili awe Kuhani Mkuu wao aliye mwaminifu na mwenye huruma katika kumtumikia Mungu, ili dhambi za watu ziondolewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Ndiyo maana ilimbidi awe kama ndugu zake kwa kila namna, ili awe Kuhani Mkuu wao aliye mwaminifu na mwenye huruma katika kumtumikia Mungu, ili dhambi za watu ziondolewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Kwa sababu hii ilibidi afanane na ndugu zake kwa kila hali, ili apate kuwa Kuhani Mkuu mwenye huruma na mwaminifu katika kumtumikia Mungu, ili pia apate kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi za watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Kwa sababu hii ilibidi afanane na ndugu zake kwa kila hali, ili apate kuwa Kuhani Mkuu mwenye huruma na mwaminifu katika kumtumikia Mwenyezi Mungu, ili pia apate kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi za watu.

Tazama sura Nakili




Waebrania 2:17
37 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, nina sababu ya kujisifu katika Kristo Yesu mbele za Mungu.


Kwa maana tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.


na kuwapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa msalaba, akiisha kuuua ule uadui kwa huo msalaba;


Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, ua adui katika nia zenu, kwa matendo yemi mabaya, amewapatanisha sasa,


na Kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu;


Maana yeye atakasae nao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;


Bassi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye nae vivyo hivyo alishiriki yayo bayo, illi kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani Shetani,


Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, illa atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu.


KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,


Yesu, aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemfanya, kama Musa nae alivyokuwa katika nyumba yake yote.


Na Musa alikuwa mwaminifu katika nyumba yake yote kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa;


Bassi, iwapo tunae kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, tujashike sana maungamo yetu.


Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuyachukua mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijuribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote, bila dhambi.


MAANA killa Kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wami Adamu amewekwa kwa ajili ya wana Adamu katika mambo yamkhusuyo Mungu, illi atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi;


ametajwa na Mungu kuwa Kuhani mkuu kwa mfano wa daraja la Melkizedeki.


awezae kuwachukulia wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe yu katika liali ya udhaifu;


Vivyo hivyo Kristo nae hakujitukuza nafsi yake kufanywa Kuhani mkuu, lakini yeye aliyenena nae: Mwana wangu ni wewe, Mimi leo nimekuzaa:


alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa Kuhani mkuu kwa jinsi ya Melkizedeki hatta milele.


Maana ilipendeza sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii, aliye mtakatifu, asiokuwa na uovu, asiokuua na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;


Maana torati yawaweka wana Adamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka Mwana, aliyekamilika hatta milele.


BASSI, katika hayo tuuayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunae kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu mbinguni,


Maana killa kuhani mkuu awekwa illi atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu nae awe na kitu akitoe.


Lakini Kristo akiisha kuwapo, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwa, kwa khema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo