Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 2:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Bassi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye nae vivyo hivyo alishiriki yayo bayo, illi kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani Shetani,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Basi, kwa vile watoto hao, kama awaitavyo, ni watu wenye mwili na damu, Yesu mwenyewe akawa kama wao na kushiriki ubinadamu wao. Alifanya hivyo ili, kwa njia ya kifo chake, amwangamize Ibilisi ambaye ana mamlaka juu ya kifo,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Basi, kwa vile watoto hao, kama awaitavyo, ni watu wenye mwili na damu, Yesu mwenyewe akawa kama wao na kushiriki ubinadamu wao. Alifanya hivyo ili, kwa njia ya kifo chake, amwangamize Ibilisi ambaye ana mamlaka juu ya kifo,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Basi, kwa vile watoto hao, kama awaitavyo, ni watu wenye mwili na damu, Yesu mwenyewe akawa kama wao na kushiriki ubinadamu wao. Alifanya hivyo ili, kwa njia ya kifo chake, amwangamize Ibilisi ambaye ana mamlaka juu ya kifo,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Basi kwa kuwa watoto wana mwili na damu, yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kifo chake, apate kumwangamiza huyo mwenye nguvu za mauti, yaani ibilisi,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Basi kwa kuwa watoto wana nyama na damu, yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kifo chake, apate kumwangamiza huyo mwenye nguvu za mauti, yaani ibilisi,

Tazama sura Nakili




Waebrania 2:14
32 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajibu, akamwambia, U kheri Simon bar Yunus; kwa kuwa nyama na damu hazikukufunulia haya, bali Baba yangu aliye mbinguni.


Kisha atawaambia na wale walio mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, kwenda katika moto wa milele, aliowekewa tayari Shetani na malaika zake:


Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.


Amin, amin, nawaambieni, Punje ya nganu isipoanguka katika inchi ikafa, hukaa katika hali ya peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.


Maana Kristo alikufa akafufuka akawa hayi tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hayi pia.


Maana yale yasiyowezekana kwa sharia, kwa kuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa ajili ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili:


nae alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, na vitu ambavyo haviko, illi avibatilishe vilivyoko;


Nisemayo ni haya, ndugu, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharihika.


Hatta ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwana wake, amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sharia,


akiisha kuziteka enzi na mamlaka, na kuzimithilisha kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.


Na bila shaka siri ya utawa ni kuu. Mungu alidhibirishwa katika mwili, alihesabiwa kuwa na wema katika roho, alionekana na malaika, alikhubiriwa katika mataifa, aliaminiwa katika ulimwengu, alichukuliwa juu katika utukufu.


na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Yesu Kristo, aliyebatili mauti na kuufunua uzima ua kutoa kuharibika, kwa ile Injili,


Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo marra moja.


Kwa biyo ajapo ulimwenguni, anena, Dhambi na toleo hukutaka, lakini mwili uliniwekea tayari:


Kwa hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, illi afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.


Na kwa kuwa aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.


Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuyachukua mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijuribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote, bila dhambi.


Na kwa sababu hii yu mjumbe wa agauo jipya, illi, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa ya katika agano la kwanza, walioitiwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.


aliyejuliwa tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifimuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu,


na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.


Usiogope mambo yatakavokupata: tazama mshitaki atawatupa baadhi yenu gerezani illi mjaribiwe, nanyi mtakuwa na mateso siku kumi. Uwe mwaminifu hatta kufa, nami nitakupa taji ya uzima.


Akamshika joka, yule nyoka wa zamani, aliye msingiziaji, Shetani, akamfunga miaka elfu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo