Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 13:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo bawakupata faida.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Msipeperushwe huku na huku kwa mafundisho tofauti ya kigeni. Neema ya Mungu ndiyo inayoimarisha roho zetu na wala si masharti juu ya chakula; masharti hayo hayakumsaidia kamwe mtu yeyote aliyeyafuata.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Msipeperushwe huku na huku kwa mafundisho tofauti ya kigeni. Neema ya Mungu ndiyo inayoimarisha roho zetu na wala si masharti juu ya chakula; masharti hayo hayakumsaidia kamwe mtu yeyote aliyeyafuata.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Msipeperushwe huku na huku kwa mafundisho tofauti ya kigeni. Neema ya Mungu ndiyo inayoimarisha roho zetu na wala si masharti juu ya chakula; masharti hayo hayakumsaidia kamwe mtu yeyote aliyeyafuata.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Msichukuliwe na kila aina ya mafundisho ya kigeni. Ni vyema mioyo yenu iimarishwe kwa neema, wala si kwa sheria kuhusu utaratibu wa vyakula, ambavyo havina faida kwa wale wanaozishika hizo sheria.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Msichukuliwe na kila aina ya mafundisho ya kigeni. Ni vyema mioyo yenu iimarishwe kwa neema, wala si kwa sheria kuhusu utaratibu wa vyakula, ambavyo havina faida kwa wale wanaozishika hizo sheria.

Tazama sura Nakili




Waebrania 13:9
35 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana wataondoka Makristo ya uwongo, na manabii ya uwongo, nao watafanyiza ishara kubwa ua mataajabu; wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wateule.


Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganyeni.


Lakini divai mpya sharti kutiwa katika viriba vipya.


tena katika baadhi yenu wataondoka watu, wakisema mapotofu, wawavute wanafunzi kwenda nyuma yao.


Bassi, sasa ndugu, nawawekeni katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, kwake yeye awezae kuwajengeni na kuwapeni urithi pamoja nao wote waliotakasika.


Maana ufalme wa Muugu si kula na kunywa, bali baki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.


Mtu mmoja ana imani, anakula vyote, lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.


Yeye aadhimishae siku, kwa Bwana aiadhimisha; na yeye asiyeadhimisha siku, haiadhimishi kwa Bwana; nae alae, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; nae asiokula, hali kwa Bwana, nae amshukuru Mungu.


Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu ataharibu vyote viwili, tumbo na vyakula. Na mwili si kwa zina, hali ni kwa Bwana, nae Bwana ni kwa mwili.


Lakini chakula hakituleti mbele ya Mungu; maana, tukila, hatuongezewi kitu, na tusipokula hatupunguziwi kitu.


Bassi Yeye atufanyae imara pamoja na ninyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu,


NDUGU, mtu ajapogbafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrudini mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako nsijaribiwe wewe mwenyewe.


illi tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukulivva kwa killa upepo wa elimu, kwa bila ya watu, kwa ujanja, tukifuata njia za udanganyifu;


Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo maana; maana kwa sababu ya haya ghadhabu ya Mungu huwajia wana wa uasi.


Nasema neno hili, mtu asije akawadanganyeni kwa maneno yaliyotungwa illi kuwakosesha.


awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika killa neno na tendo jema.


msifadhaishwe upesi na kuaeha nia yenu, wala msistushwe, kwa roho wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, ya kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.


Timotheo, ilinde amana, ukijiepisha na maneno yasiyo ya dini, yasiyo maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa nwongo;


WAPENZI, msiamini kiila rolio, bali zijaribuni roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uwongo wengi wametokea duniani.


Watu hawa ni miamba yenye khatari katika karamu zenu za upendo wafanyapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo khofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa marra mbili, na kungʼolewa kabisa;


Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia khabari ya wokofu wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikieni, illi niwaonye mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu marra moja tu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo