Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 13:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Wakumbukeni wale waliokuwa na mamlaka juu yenu, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa maisha zao, iigeni imani yao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni neno la Mungu. Fikirini juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni neno la Mungu. Fikirini juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni neno la Mungu. Fikirini juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Wakumbukeni viongozi wenu, wale waliowaambia neno la Mungu. Angalieni matokeo ya mwenendo wa maisha yao mkaiige imani yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Wakumbukeni viongozi wenu, wale waliowaambia neno la Mwenyezi Mungu. Angalieni matokeo ya mwenendo wa maisha yao mkaiige imani yao.

Tazama sura Nakili




Waebrania 13:7
27 Marejeleo ya Msalaba  

Nani bassi aliye mtumishi yule amini mwenye haki, ambae bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape chakula kwa saa yake?


Bwana akasema, Nani, bassi, aliye wakili mwaminifu niwenye busara, ambae Bwana wake atamweka juu ya ntumishi wake wote, awape watu posho lao kwa saa yake?


IKAWA makutano walipomsonga, wakisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa akisimama kando ya ziwa la Genesareti:


Na mfano ndio huu: Mbegu ni neno la Mungu.


Paolo na Barnaba wakanena kwa uthabiti wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza: illakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, wala hamjioni nafsi zenu kuwa mmestahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia mataifa.


Na walipokwisha kuchagua wazee katika killa mji, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka kafika mikono ya Bwana waliyemwamini.


Hatta walipokwisha kumwomba Mungu, pahali paie walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa uthabiti.


Bassi imani, chanzo chake ni kusikla; na kusikia kunakuja kwa neno la Mungu.


Jaribu halikuwapata ninyi, illa ya kadiri ya kibinadamu; na Mungu yu amini; hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, illi mweze kustahimili.


MWE wafuasi wangu kama mimi nilivyo mfuasi wa Kristo.


Bassi, nawasihini, mwe wafuasi wangu.


Mwe wafuasi wangu, ndugu, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliokupeni.


Mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea Neno katika mateso mengi pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu,


Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa mlipopokea lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la kibinadamu; bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli, litendalo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.


Mwajua wenyewe jinsi iwapasavyo kutufuata, kwa sababu hatukwenda bila utaratibu kwenu;


si kwamba hatuna uwezo, bali tufanye nafsi zetu kuwa mfano kwenu, mtufuate.


(mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje kanisa la Mungu?)


Watiini walio na mamlaka juu yenu, na kujinyenyekea kwao; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, illi wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.


Wasalimuni wote walio na mamlaka juu yenu, na watakatifu wote; walio wa Italia wanakusalimuni.


illi msiwe wavivu, hali wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imaui na uvumilivu.


Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akikhudumu, na akhudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; illi Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo; utukufu na uweza u kwake hatta milele na milele. Amin.


Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.


Nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, wakapewa hukumu: nikaona roho zao waliokatwa kichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia nyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea alama yake katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; wakawa hayi, wakamiliki pamoja na Kristo miaka elfu.


Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhbahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo