Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 13:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Msiwe na tabia ya kupenda fedha: mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema: “Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema: “Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema: “Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Yalindeni maisha yenu msiwe na tabia ya kupenda fedha, bali mridhike na vile mlivyo navyo, kwa sababu Mungu amesema, “Kamwe sitakuacha, wala sitakupungukia.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Yalindeni maisha yenu msiwe na tabia ya kupenda fedha, bali mridhike na vile mlivyo navyo, kwa sababu Mungu amesema, “Kamwe sitakuacha, wala sitakupungukia.”

Tazama sura Nakili




Waebrania 13:5
46 Marejeleo ya Msalaba  

Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu ziharibupo, na wevi huvunja na kuiba:


Kiva sababu hii nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mleni au mnyweni; wala mwili wenu, mvaeni. Maisha je, si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?


Bassi msisumbukie kesho; kwa kuwa kesho itayasumbukia mambo yake. Watosba kwa siku ubaya wake.


wizi, uuaji, tamaa mbaya, hila, jeuri, kijicho, matukano, kiburi, upumbafu.


Askari nao wakamwuliza wakisema, Nasi tufanyeni? Akawaambia, Msimtende jeuri mtu aliye yote, wala msitoze kitu bila haki; tena mwe radhi na mshsahara wenu.


Nazo zilizoangukia miibani, hawa ndio waliosikia, nao wakienda zao husongwa na shughuli, na mali, na anasa za maisha, wasizae kwa utimilifu.


wakijawa na udhalimu wa killa namna ya zina, na novu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na khadaa;


Lakini sasa nimewaandikieni kwamba msichangamane na mtu aitwae ndugu, akiwa mzinzi au mwenye kutamani an mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnangʼanyi; mtu wa namna hii msikubali hatta kula nae.


wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyangʼanyi.


twatupwa chini, bali hatuangamizwi;


Lakini uasharati na uchafu wote au kutamani kusinenwe kwenu kabisa, kama iwastahilivyo watakatifu;


Maana neno hili mnalijua kwa kulifaliamu, kwamba hapana asharati, wala mchafu, wala mtu wa tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.


Bassi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika inchi, uasharati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu:


si mtu wa kuzoelea mvinyo, si mpigaji, si mtu apendae fedha; bali awe mpole, asiwe mtu wa kujadiliana, asitamani fedha;


wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kukhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo ilivozoezwa kutamani, wana wa laana;


Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa: hukumu yao tangu zamani haikawii, wala upotevu wao hausinzii.


Ole wao! kwa sababu walikwenda katika njia ya Kain, na kulifuata kosa la Balaam pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo