Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 13:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 awafanye kuwa wrakamilifu katika killa tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, nae akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amin.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Mungu wa amani awakamilishe katika kila tendo jema ili mtekeleze matakwa yake; yeye na afanye ndani yetu kwa njia ya Kristo yale yanayompendeza mwenyewe. Utukufu uwe kwake, milele na milele! Amina.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Mungu wa amani awakamilishe katika kila tendo jema ili mtekeleze matakwa yake; yeye na afanye ndani yetu kwa njia ya Kristo yale yanayompendeza mwenyewe. Utukufu uwe kwake, milele na milele! Amina.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Mungu wa amani awakamilishe katika kila tendo jema ili mtekeleze matakwa yake; yeye na afanye ndani yetu kwa njia ya Kristo yale yanayompendeza mwenyewe. Utukufu uwe kwake, milele na milele! Amina.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 awafanye ninyi wakamilifu mkiwa mmekamilishwa katika kila jambo jema ili mpate kutenda mapenzi yake, naye atende ndani yetu kile kinachompendeza machoni pake, kupitia kwa Isa Al-Masihi, ambaye utukufu una yeye milele na milele. Amen.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 awafanye ninyi wakamilifu mkiwa mmekamilishwa katika kila jambo jema ili mpate kutenda mapenzi yake, naye atende ndani yetu kile kinachompendeza machoni Pake, kwa njia ya Isa Al-Masihi, ambaye utukufu una yeye milele na milele. Amen.

Tazama sura Nakili




Waebrania 13:21
53 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana ye yote atakaeyafanya mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.


Katika hawa wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya baba yake? Wakamwambia, Yule wa kwanza. Yesu akawaambia, Amin, nawaambieni, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.


mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi: nti tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hatta mwisho wa dunia. Amin.


Usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu.


Siye killa mtu aniambiae, Bwana, Bwana, atakaeingia katika ufalme wa mbinguni; hali yeye afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.


mimi ndani yao, na wewe ndani yangu, wapate kukamilika na kuwa umoja; illi ulimwengu ujue ya kuwa udiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.


Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua khabari ya elimu hii kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.


Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amin.


yeye ndiye Mungu mwenye hekima peke yake; na atukuzwe kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amin.


Na Mungu aweza kuwajaza killa neema kwa wingi, illl ninyi, mkiwa na riziki za killa namna siku zote, mpate kuzidi sana katika killa tendo jema;


ambae ana utukufu milele na milele, Amin.


Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo Mungu aliyatengeneza tokea awali illi tuenende nayo.


Maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Mungu Baba katika Roho mmoja.


mmejazwa matuuda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.


killa ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.


kwa maana ni Mungu atendae ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa ajili ya kusudi lake jema.


Nayaweza mambo yote katika yeye anitiae nguvu.


Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi; tena nimejaa tele, nimepokea kwa mkono ya Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.


Na killa mfanjalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.


Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jamlio hili lapendeza katika Bwana.


Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu, katika maombi yake msimame wakamilifu mkathuhutike sana katika mapenzi yote ya Mungu.


apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwaua wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.


Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na nasharati;


Mungu wa amani mwenyewe awatakase kahisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.


awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika killa neno na tendo jema.


Kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu wa hekima peke yake, kwake yeye heshima na utukufu milele na milele. Amin.


na kushuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata killa tendo jema.


ambae yeye peke yake hapatikani na mauti, akaae katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hapana mwana Adamu aliyemwona, wala awezae kumwona, ndiye mwenye heshima na uweza milele. Amin.


illi mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa illi atende killa tendo jema.


Na Bwana ataniokoa na killa neno baya na kunihifadhi hatta uje ufalme wake wa milele.


Maana mnahitaji uvumilivu, illi mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu muipate abadi.


na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,


Bassi tukipokea ufalme usioweza kutetemeshwa, tuwe na neema, illi kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho:


Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana na watu; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.


ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hayi, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani utakatifu, mtoe dhabibu za roho, zipatazo kibali kwa Mungu, kwa Yesu Kristo.


kuanzia sasa tusiendelee kuishi katika tamaa za wana Adamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wetu wa kukaa hapa duniani uliobakia.


Lakini, kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hatta milele. Amin.


Na dunia inapita, na tamaa yake, bali yeye afanyae mapenzi ya Mungu adumu hatta milele.


na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.


Yeye aliye Mungu pekee, mwenye hekima, Mwokozi wetu: kwake yeye utukufu, na ukuu, na uwezo, na nguvu kwa Yesu Kristo, tangu milele, na sasa, na hatta milele. Amin.


Na mliele ya kile kiti cha enzi, mfano wa bahari ya kioo eheupe, kama krustallo, na kati kati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, nyama wane, wamejaa macho mbele na nyuma.


Na killa kiumbe kilicho mbinguni na juu ya inchi na chini ya inchi na juu ya bahari, na vitu vyote vilivyo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na una Mwana Kondoo hatta milele na milele.


Nao waimba uimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulicbinjwa


Tufuate:

Matangazo


Matangazo