Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 13:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 Bassi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka wafu Mchungaji wa kondoo aliye mkuu, kwa damu ya agano la milele, Bwana wetu Yesu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Mungu amemfufua katika wafu Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mchungaji Mkuu wa kondoo kwa sababu ya kumwaga damu yake iliyothibitisha agano la milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Mungu amemfufua katika wafu Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mchungaji Mkuu wa kondoo kwa sababu ya kumwaga damu yake iliyothibitisha agano la milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Mungu amemfufua katika wafu Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mchungaji Mkuu wa kondoo kwa sababu ya kumwaga damu yake iliyothibitisha agano la milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Basi Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya agano la milele alimleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Isa, yule Mchungaji Mkuu wa kondoo,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Basi Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya Agano la milele alimleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Isa, yule Mchungaji Mkuu wa kondoo,

Tazama sura Nakili




Waebrania 13:20
53 Marejeleo ya Msalaba  

maana hii ni damu yangu ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.


Akawaambia, Hii ni damu yangu, ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya watu wengi.


Nacho kikombe vivyo hivyo baada ya kula, akinena, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.


Mimi ndimi niliye mchunga aliye mwema: mchunga aliye mwema huweka maisha yake kwa ajili ya kondoo.


Mimi ndimi niliye mchunga aliye mwema; na walio wangu nawajua, na walio wangu wananijua,


Lakini Mungu akamfufua:


Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa ujumbe wa mtu yule aliyemchagua; nae amewapa watu wote bayana ya mambo haya kwa kumfufua katika wafu.


Mungu akamfufua, akilegeza utungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.


Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake.


mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambae Mungu amemfufua: na sisi tu mashahidi wake.


jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Mnazareti, ambae ninyi mlimsulibisha, Mungu akamfufua, kwa jina hilo mtu huyu anasimama mzima mbele yenu.


Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambae ninyi mlimwua mkamtundika katika mti.


na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo; Yesu Kristo Bwana wetu,


au, Ni nani atakaeshuka kuzimuni? (yaani, ni kuleta Kristo juu, kutoka kwa wafu.)


Mungu wa amani awe pamoja nanyi nyote. Amin.


Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu kwa upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.


Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu ataihuisha na miili yemi iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho yake anayekaa ndani yenu.


Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.


Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uwongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambae hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.


Na Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua na sisi kwa uweza wake.


Khatimae, ndugu, kwa kherini; mtimilike, mfarajike, nieni mamoja, mkae katika imani; na Mungu wa upendo na amani awe pamoja nanyi.


tukijua kama yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua na sisi pamoja na Yesu, na kutuhudhurisha pamoja nanyi.


PAOLO, mtume (si mtume wa wana Adamu, wala hakutumwa na mwana Adamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua),


aliyotenda katika Kristo alipomfufua, akamweka mkono wake wa kuume katika mbingu,


Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia, na kuyaona kwangu, yatendeni haya; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.


mkizikwa pamoja nae katikti ubatizo, katika huo mlifufuliwa pamoja nae, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.


na kumugojea Mwana wake kutoka mbinguni, ambae alimfufua katika wafu, Yesu, anaetuokoa na ghadhabu itakayokuja.


Mungu wa amani mwenyewe awatakase kahisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.


Sasa, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani siku zote kwti njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.


tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa mwili kwa maji safi.


Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa nayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho ya neema?


akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu.


ambae kwa yeye mlimwamini Mungu, aliyemfufua akampa utukufu; hatta imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.


Kwa maana mlikuwa kama kondoo wanaopotea; lakini sasa mmemrudia Mchunga na Askofu wa roho zenu.


Na mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo