Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 13:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Msisahau kuwafadhilia wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Msisahau kuwakaribisha wageni; maana kwa kufanya hivyo watu wengine walipata kuwakaribisha malaika bila kujua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Msisahau kuwakaribisha wageni; maana kwa kufanya hivyo watu wengine walipata kuwakaribisha malaika bila kujua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Msisahau kuwakaribisha wageni; maana kwa kufanya hivyo watu wengine walipata kuwakaribisha malaika bila kujua.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Msisahau kuwakaribisha wageni, kwa kuwa kwa kufanya hivyo, watu wengine waliwakaribisha malaika pasipo kujua.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Msisahau kuwakaribisha wageni, kwa kuwa kwa kufanya hivyo, watu wengine waliwakaribisha malaika pasipo kujua.

Tazama sura Nakili




Waebrania 13:2
21 Marejeleo ya Msalaba  

kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;


Na mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambieni. Kadiri mlivyomtendea mmojawapo katika hawo ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.


nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike: nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.


Hatta alipokwisha kumbatiza, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae; akatushurutisha.


kwa mahitaji ya watakatifu, mkiwashirikisha; katika kukaribisha wageni, mkijitahidi.


Gayo, mwenyeji wangu na wa Kanisa lote pia awasalimu. Erasto, wakili wa mji awasalimu, na Kwarto, ndugu yetu.


Bassi imempasa askofu kuwa mtu asiyelaumiwa, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, mfundishaji;


na kushuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata killa tendo jema.


bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kujimudu nafsi yake;


mwe wakaribishaji ninyi kwa ninyi, pasipo kunnngʼunika;


Mpenzi, kazi ile ni ya naminifu uwatendeayo ndugu na wageni,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo