Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 13:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Watiini walio na mamlaka juu yenu, na kujinyenyekea kwao; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, illi wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Watiini viongozi wenu na kushika amri zao; wao huchunga roho zenu usiku na mchana, na watatoa ripoti ya utumishi wao mbele ya Mungu. Kama mkiwatii watafanya kazi zao kwa furaha, la sivyo, watazifanya kwa huzuni, na hiyo haitakuwa na faida kwenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Watiini viongozi wenu na kushika amri zao; wao huchunga roho zenu usiku na mchana, na watatoa ripoti ya utumishi wao mbele ya Mungu. Kama mkiwatii watafanya kazi zao kwa furaha, la sivyo, watazifanya kwa huzuni, na hiyo haitakuwa na faida kwenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Watiini viongozi wenu na kushika amri zao; wao huchunga roho zenu usiku na mchana, na watatoa ripoti ya utumishi wao mbele ya Mungu. Kama mkiwatii watafanya kazi zao kwa furaha, la sivyo, watazifanya kwa huzuni, na hiyo haitakuwa na faida kwenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Watiini viongozi wenu na kujinyenyekeza chini ya mamlaka yao. Kwa maana wao wanakesha kwa ajili yenu kama watu watakaopaswa kutoa maelezo. Watiini ili wafanye kazi yao kwa furaha, wala si kama mzigo, maana hiyo haitakuwa na faida kwenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Watiini viongozi wenu na kujinyenyekeza chini ya mamlaka yao. Kwa maana wao wanakesha kwa ajili yenu kama watu watakaopaswa kutoa hesabu. Watiini ili wafanye kazi yao kwa furaha, wala si kama mzigo, maana hiyo haitakuwa na faida kwenu.

Tazama sura Nakili




Waebrania 13:17
34 Marejeleo ya Msalaba  

Akamwita, akamwambia, Nini hii nisikiayo juu yako? Toa khabari ya uwakili wako, maana huwezi tena kuwa wakili.


Jiangalieni nafsi zenu, na kundi lote, ambalo Roho Mtakatifu aliwakabidhi mlisimamie, kanisa lake Mungu, alilojipatia kwa damu yake mwenyewe.


Bassi kama ni hivyo, killa mtu miongoni mwetu atatoa khabari za nafsi yake mbele za Mungu.


bassi watiini watu kama hawa, na killa mtu afanyae kazi pamoja nao, na kujitaabisha.


mkitumikiana katika khofu ya Kristo.


siku zote killa niwaombeapo ninyi nyote nikisema sala zangu kwa furaha,


Bassi, wapendwa, kama vile mlivyotii siku zote, si wakati mimi nilipokuwapo, bali sasa zaidi mimi nisipokuwapo, utimizeni wokofu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka;


nipate sababu ya kujisifu katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio burre wala sikujitaabisha burre.


Mpokeeni, bassi, katika Bwana, kwa furaha yote, mkawahesabu watu kama huyu kuwa watu wa kuheshimiwa.


Maana wengi huenenda, nimewaambieni marra nyingi khabari zao, na hatta sasa nawaambieni kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;


BASSI, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu.


Na ikiwa mtu aliye yote halishiki neno letu la waraka huu, jihadharini na mtu huyo, wala msizumgumze nae, apate kutahayarika;


Wazee watawalao vema wapewe heshima mardufu, khassa wao wajitaabishao kwa kukhutubu na kufundisha.


Wasalimuni wote walio na mamlaka juu yenu, na watakatifu wote; walio wa Italia wanakusalimuni.


Wakumbukeni wale waliokuwa na mamlaka juu yenu, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa maisha zao, iigeni imani yao.


Bassi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, nae atawakimbia.


Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu kama mshipi, mpate kukhudumiana; kwa sababu Mungu hushindana na wenye kiburi, huwapa wanyenyekevu neema.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo