Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 13:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Bassi na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo ya watu waliungamao jina lake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Basi, kwa njia ya Yesu, tumtolee Mungu tambiko ya sifa daima, yaani sifa zinazotolewa kwa midomo inayoliungama jina lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Basi, kwa njia ya Yesu, tumtolee Mungu tambiko ya sifa daima, yaani sifa zinazotolewa kwa midomo inayoliungama jina lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Basi, kwa njia ya Yesu, tumtolee Mungu tambiko ya sifa daima, yaani sifa zinazotolewa kwa midomo inayoliungama jina lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Basi kupitia kwa Isa, tuzidi kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani matunda ya midomo inayolikiri Jina lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Basi kwa njia ya Isa, tuzidi kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani matunda ya midomo inayolikiri Jina lake.

Tazama sura Nakili




Waebrania 13:15
42 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati ule Yesu akajibu akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa uliwaficha haya wenye hekima na busara, ukawafunulia wadogo:


Saa ileile Yesu akashangilia katika Roho, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa umewaficha wenye hekima na busara mambo haya, ukawafunulia watoto wachanga: Naam, Baba, kwa maana ndivyo vilivyokuwa vinapendeza mbele yako.


Mimi ndimi niliye mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka, ataingia, atatoka, na atapata malisho.


Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.


BASSI, nawasihi, ndugu, kwa huruma zake Mungu, mtoe miili yenu iwe dhabihu hayi, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ibada yenu yenye maana.


Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa maana kama mlivyotoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na maasi mpate kuasi, vivyo sasa toeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa.


Maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Mungu Baba katika Roho mmoja.


mkimshukuru Baba, aliyetustahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru;


Bassi tukipokea ufalme usioweza kutetemeshwa, tuwe na neema, illi kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho:


Nae, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye; maana yu hayi siku zote illi awaombee.


ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hayi, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani utakatifu, mtoe dhabibu za roho, zipatazo kibali kwa Mungu, kwa Yesu Kristo.


Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akikhudumu, na akhudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; illi Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo; utukufu na uweza u kwake hatta milele na milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo