Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 12:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Maana mtafakarini sana yeye aliyeyavumilia mapingamizi makuu namna hii ya wenye dhambi juu ya nafsi zao, msije mkadhoofika mkizimia mioyoni mwenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Fikirini juu ya mambo yaliyompata Yesu, jinsi alivyostahimili upinzani mkubwa kwa watu wenye dhambi. Basi, msife moyo, wala msikate tamaa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Fikirini juu ya mambo yaliyompata Yesu, jinsi alivyostahimili upinzani mkubwa kwa watu wenye dhambi. Basi, msife moyo, wala msikate tamaa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Fikirini juu ya mambo yaliyompata Yesu, jinsi alivyostahimili upinzani mkubwa kwa watu wenye dhambi. Basi, msife moyo, wala msikate tamaa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Mtafakarini sana yeye aliyestahimili upinzani mkuu namna hii kutoka kwa watu wenye dhambi, ili msije mkachoka na kukata tamaa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Mtafakarini sana yeye aliyestahimili upinzani mkuu namna hii kutoka kwa watu wenye dhambi, ili kwamba msije mkachoka na kukata tamaa.

Tazama sura Nakili




Waebrania 12:3
46 Marejeleo ya Msalaba  

Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakanena, Mlafi huyu, na mnywa mvinyo, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imepewa haki na watoto wake.


Lakini Mafarisayo waliposikia, wakasema, Huyu hafukuzi pepo, illa kwa uweza wa Beelzebul mkuu wa pepo.


Mbona wanafunizi wako huyakhalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula.


Hatta alipokwisha kuingia hekaluni, makuhani wakuu na wazee wa watu wakamwendea alipokuwa akifundisha, wakinena, Kwa mamlaka gani unafanya haya? Na nani aliyekupa mamlaka haya?


Nao walipotafuta kumkamata, wakawaogopa makutano, kwa maana walimwona kuwa nabii.


Ndipo Mafarisayo wakaenda zao, wakafauya shauri, jinsi ya kumtega kwa maneno.


IKAWA, Yesu alipoingia katika nyumba ya mtu mmoja, mtu mkuu katika Mafarisayo, siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia.


Mafarisayo na wandishi wakanungʼunika, wakasema, Huyu hukaribisha wenye dhambi, hula pamoja nao.


Mafarisayo nao wakayasikia haya yote, nao walikuwa wakipenda fedha; wakamdhihaki.


Sumeon akawabariki, akamwambia Mariamu, mama yake, Hakika huyu amewekwa, waanguke, wasimame wengi katika Israeli; awe ishara inenwayo;


Wale waandishi na Mafarisayo wakaanza kutafakari wakanena, Nani huyu anaesema kufuru? Nani awezae kuondoa dhambi, isipokuwa mmoja ndiye Mungu?


Wengi wao wakasema, Ana pepo, tena ana wazimu; mbona mnamsikiliza?


Aliposema maneno haya, mmoja wa wale watumishi aliyesimama karibu akampiga Yesu koli, akinena, Wamjibu hivi kuhani mkuu?


Kwa sababu hiyo Wayahudi wakaanza kumwudhi Yesu, wakitaka kumwua, kwa kuwa alitenda haya siku ya sabato.


Kukawa manungʼuniko mengi katika makutano kwa khabari zake; wengine wakisema, Yu mtu mwema; na wengine wakisema, Sivyo, bali anawadanganya makutano.


Bassi Mafarisayo wakamwambia, Wewe unajishuhudia nafsi yako; ushuhuda wako si kweli.


Bassi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumefahamu ya kuwa una pepo; Ibrahimu amekufa na manabii, na wewe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti kabisa hatta milele.


Bassi wakatwaa mawe wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.


Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pamoja nae wakasikia haya, wakamwambia, Je! sisi nasi tu vipofu?


Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana.


KWA sababu hiyo, kwa kuwa tuna khuduma hii, kwa jinsi tulivyorehemiwa, hatulegei;


Kwa hiyo hatuzimii; bali ijapokuwa mtu wetu wa nje unaharibiwa, illakini mtu wetu wa ndani unafanywa npya siku baada ya siku.


Na tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia.


Lakini, ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema.


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama na wana. Mwanangu, usikudharau kurudi kwake Bwana, Wala, usizimie ukikemewa nae;


KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,


yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki;


tena ulistahimili na kuwa na uvumilivu, na kwa ajili yangu umejitaabisha wala hukuchoka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo