Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 12:27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

27 Neno lile, Marra moja tena, ladhihirisha kuhamishwa vile viwezavyo kutetemeshwa, kama vitu vilivyoumbwa, illi vitu visivyoweza kutetemeshwa vikae.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Neno hili: “Tena” linatuonesha kwamba vitu vyote vilivyoumbwa vitatetemeshwa na kutoweka ili vibaki vile visivyotetemeshwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Neno hili: “Tena” linatuonesha kwamba vitu vyote vilivyoumbwa vitatetemeshwa na kutoweka ili vibaki vile visivyotetemeshwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Neno hili: “tena” linatuonesha kwamba vitu vyote vilivyoumbwa vitatetemeshwa na kutoweka ili vibaki vile visivyotetemeshwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Maneno haya “kwa mara moja tena” yanaonesha kuondoshwa kwa vile vitu vinavyoweza kutetemeshwa, yaani vile vitu vilivyoumbwa, kwa kusudi vile vitu visivyoweza kutetemeshwa vibaki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Maneno haya “kwa mara moja tena” yanaonyesha kuondoshwa kwa vile vitu vinavyoweza kutetemeshwa, yaani vile vitu vilivyoumbwa, kwa kusudi vile tu visivyoweza kutetemeshwa vibaki.

Tazama sura Nakili




Waebrania 12:27
19 Marejeleo ya Msalaba  

Mbingu na inchi zitapita; bali maneno yangu hayatapita kamwe.


Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi siku ile watakayofunuliwa wanawa Mungu.


katika tumaini: kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu viingie uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.


Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.


Na, wewe, Bwana, mwanzo umeitia misingi ya inchi, na mbingu ni kazi za mikono yako;


Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.


Lakini Kristo akiisha kuwapo, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwa, kwa khema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu,


Malaika wa saha akapiga baragumu, pakawa sauti kuu katika mbingu, zikisema, Falme za dunia zimekwisha kuwa ufalme na Mungu na wa Kristo wake, nae atamiliki hatta milele na milele.


NIKAONA mbingu mpya na inchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na inchi za kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.


Nae atafuta killa chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena: wala maombolezo, wala kilio, wala taabu haitakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.


Na yeye aketiye juu ya kiti cha enzi akasema, Tazama, nafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika, kwa maana haya ni maneno ya kweli, na ya uaminifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo