Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 12:25 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

25 Angalieni msimkatae yeye anenae. Maana ikiwa wale hawakuokoka waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya inchi, sembuse sisi tukijiepusha nae atuonyae kutoka mbinguni:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Basi, jihadharini msije mkakataa kumsikiliza huyo anayesema nanyi. Kama wale waliokataa kumsikiliza yule aliyewaonya hapa duniani hawakuokoka, sisi tutawezaje kuokoka kama tukikataa kumsikiliza yule anayetuonya kutoka mbinguni?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Basi, jihadharini msije mkakataa kumsikiliza huyo anayesema nanyi. Kama wale waliokataa kumsikiliza yule aliyewaonya hapa duniani hawakuokoka, sisi tutawezaje kuokoka kama tukikataa kumsikiliza yule anayetuonya kutoka mbinguni?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Basi, jihadharini msije mkakataa kumsikiliza huyo anayesema nanyi. Kama wale waliokataa kumsikiliza yule aliyewaonya hapa duniani hawakuokoka, sisi tutawezaje kuokoka kama tukikataa kumsikiliza yule anayetuonya kutoka mbinguni?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Angalieni msije mkamkataa yeye anenaye. Ikiwa wao hawakuepuka adhabu walipomkataa yeye aliyewaonya hapa duniani, sisi je, tutaokokaje tusipomsikiliza yeye anayetuonya kutoka mbinguni?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Angalieni, msije mkamkataa yeye anenaye. Ikiwa wao hawakuepuka adhabu walipomkataa yeye aliyewaonya hapa duniani, sisi je, tutaokokaje tusipomsikiliza yeye anayetuonya kutoka mbinguni?

Tazama sura Nakili




Waebrania 12:25
36 Marejeleo ya Msalaba  

Alipokuwa akisema, wingu jeupe likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, niliyependezwa nae; msikieni yeye.


Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; illa enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, utoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.


Musa huyo waliyemkataa, wakisema, Ni nani aliyekuweka kuwa mkuu na mwamuzi? ndiye aliyetumwa na Mungu kuwa mkuu na mkombozi, kwa mkono wa yule malaika aliyemtokea katika kile kijiti.


Angalieni mtu awae yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.


nao watajiepusha na kusikia yaliyo kweli watageukia hadithi za uwongo.


KWA sehemu nyingi na kwa namna nyingi Mungu zamani alisema na babu zetu katika manabii,


Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu khabari za mambo yasiyoonekana bado, kwa kumcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Kwa hiyo akauhukumu ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.


ambayo wale waliosikia walisihi wasiambiwe neno lo lote lingine; maana hawakuweza kustahimili neno lile lililoamriwa,


Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hayi.


Na ni nani aliochukizwa nao miaka arubaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?


watumikao kwa mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile khema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.


Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;


Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.


Akaniambia, Angalia, usifanye hivyo; mimi mjoli wako, na wa ndugu zako manabii na wa wale washikao maneno ya kitabu hiki. Msujuduni Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo