Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 12:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 na Yesu mwenye kuleta agano jipya, na damu ya kunyunyizwa inenayo mema kuliko ile ya Habil.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Mmefika kwa Yesu ambaye ni mpatanishi katika agano jipya, na ambaye damu yake iliyomwagika inasema mambo mema kuliko ile ya Abeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Mmefika kwa Yesu ambaye ni mpatanishi katika agano jipya, na ambaye damu yake iliyomwagika inasema mambo mema kuliko ile ya Abeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Mmefika kwa Yesu ambaye ni mpatanishi katika agano jipya, na ambaye damu yake iliyomwagika inasema mambo mema kuliko ile ya Abeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 kwa Isa mpatanishi wa agano jipya, na kwa damu iliyonyunyizwa, ile inenayo mambo mema kuliko damu ya Habili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 kwa Isa mpatanishi wa agano jipya, na kwa damu iliyonyunyizwa, ile inenayo mambo mema kuliko damu ya Habili.

Tazama sura Nakili




Waebrania 12:24
24 Marejeleo ya Msalaba  

illi iwajieni damu yote ya haki iliyomwagika katika inchi, tangu damu ya Habil, yule mwenye haki, hatta damu ya Zakaria, mwana wa Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhbahu,


maana hii ni damu yangu ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.


Akawaambia, Hii ni damu yangu, ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya watu wengi.


tangu damu ya Habil hatta damu ya Zakaria aliyeuawa kati ya madhhahu na patakatifu. Naam, nawaambieni, itatakwa kwa kizazi hiki.


Nacho kikombe vivyo hivyo baada ya kula, akinena, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.


Aliye mjumbe si mjumbe wa mmoja; bali Mungu ni mmoja.


Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wana Adamu ni mmoja, mwana Adamu, Kristo Yesu,


tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa mwili kwa maji safi.


Kwa imani akaifanya Pasaka, na kunyunyiza ile damu, illi mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao.


Kwa imani Habil alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kain; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo ijapokuwa amekufa, angali akinena.


Bassi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka wafu Mchungaji wa kondoo aliye mkuu, kwa damu ya agano la milele, Bwana wetu Yesu,


bassi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo hora zaidi.


Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikukuu na kuchakaa ni karibu na kutoweka.


Lakini sasa amepata khuduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mtengenezaji wa agano lililo bora, lililoamriwa kwa ahadi zilizo bora na kuzitegemea.


Maana, awalaumupo, asema, Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya; halitakuwa kama agano lile nililofanyana na baba zao, katika siku ile nilipowashika mikono yao uiwatoe katika inchi ya Misri.


Na kwa sababu hii yu mjumbe wa agauo jipya, illi, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa ya katika agano la kwanza, walioitiwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.


Maana killa amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa watu wote, kama ilivyoamuru sharia, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi pamoja na maji na sufu nyekundu na husopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote,


Na ile khema na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivi hivi.


kama vile Mungu alivyotangulia kuwajua tangu milele katika utakaso wa Roho, hatta wakapata kutii na kunyunyizwa damu ya Yesu Kristo; Neema na amani ziongezwe kwenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo