Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 12:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Mmefika kwenye kusanyiko kubwa la wazaliwa wa kwanza wa Mungu, ambao majina yao yameandikwa mbinguni. Mnasimama mbele ya Mungu aliye hakimu wa wote, na mbele ya roho za watu waadilifu waliofanywa wakamilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Mmefika kwenye kusanyiko kubwa la wazaliwa wa kwanza wa Mungu, ambao majina yao yameandikwa mbinguni. Mnasimama mbele ya Mungu aliye hakimu wa wote, na mbele ya roho za watu waadilifu waliofanywa wakamilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Mmefika kwenye kusanyiko kubwa la wazaliwa wa kwanza wa Mungu, ambao majina yao yameandikwa mbinguni. Mnasimama mbele ya Mungu aliye hakimu wa wote, na mbele ya roho za watu waadilifu waliofanywa wakamilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 kwenye jumuiya ya waumini ya wazaliwa wa kwanza wa Mungu, ambao majina yao yameandikwa mbinguni. Mmekuja kwa Mungu, mhukumu wa watu wote, kwenye roho za wenye haki waliokamilishwa,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 kwenye jumuiya ya waumini ya wazaliwa wa kwanza wa Mwenyezi Mungu, ambao majina yao yameandikwa mbinguni. Mmekuja kwa Mwenyezi Mungu, mhukumu wa watu wote, kwenye roho za wenye haki waliokamilishwa,

Tazama sura Nakili




Waebrania 12:23
45 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini msifurahi kwa sababu hii ya kuwa pepo wanawatiini: hali furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa mbinguni.


akampa mamlaka ya kufanya hukumu kwa sababu yu Mwana wa Adamu.


Jiangalieni nafsi zenu, na kundi lote, ambalo Roho Mtakatifu aliwakabidhi mlisimamie, kanisa lake Mungu, alilojipatia kwa damu yake mwenyewe.


Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule uso kwa uso: wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana jinsi ninavyojuliwa na mimi sana.


Na kama tulivyoichukua sura yake wa udongo, kadhalika tulaichukua sura yake wa mbinguni.


Bassi, uharibifu huu utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.


Lakini tuna moyo mkuu; na tunaona vema zaidi kutoka katika mwili na kukaa pamoja na Bwana.


akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajiii ya kanisa,


Naam, nakutaka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi nae, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.


mkimshukuru Baba, aliyetustahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru;


Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena natimiliza yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo katika mwili wangu, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake,


(mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje kanisa la Mungu?)


Kwa imani Habil alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kain; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo ijapokuwa amekufa, angali akinena.


kwa kuwa Mungu ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, illi wasikamilishwe pasipo sisi.


akinena, Nitalikhubiri jina lako kwa ndugu zangu; kati kati ya kanisa nitakuimba,


Na jinsi watu wanavyowekewa kufa marra moja, na baada ya kufa hukumu:


Alipopenda alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limhuko la viumbe vyake.


yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki;


Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia.


Hawa udio wasiotiwa najis pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana kondoo killa aendako. Hawa walinunuliwa katika inchi, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana kondoo.


Na ikiwa mtu hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.


Wakapewa killa mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hatta itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao watakaouawa vile vile kama wao.


Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhbahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo