Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 12:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Tumwelekee Yesu ambaye ndiye aliyeianzisha imani yetu na ambaye ataikamilisha. Kwa ajili ya furaha iliyokuwa inamngojea, yeye alivumilia kifo msalabani, bila kuijali aibu yake, na sasa anaketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Tumwelekee Yesu ambaye ndiye aliyeianzisha imani yetu na ambaye ataikamilisha. Kwa ajili ya furaha iliyokuwa inamngojea, yeye alivumilia kifo msalabani, bila kuijali aibu yake, na sasa anaketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Tumwelekee Yesu ambaye ndiye aliyeianzisha imani yetu na ambaye ataikamilisha. Kwa ajili ya furaha iliyokuwa inamngojea, yeye alivumilia kifo msalabani, bila kuijali aibu yake, na sasa anaketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Basi na tumtazame sana Isa mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu, yeye ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahimili msalaba, bila kujali aibu ya huo msalaba, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Basi na tumtazame sana Isa mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu, yeye ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahimili msalaba, bila kujali aibu ya huo msalaba, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili




Waebrania 12:2
78 Marejeleo ya Msalaba  

Toka wakati huo Yesu akaanza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemi, na kuteswa mengi na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.


kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kukhudumiwa, bali kukhudumu, na kutoa roho yake kuwa dia ya wengi.


Akasema, Abba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikomhe hiki: walakini, si nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.


Bassi andiko likatimizwa linenalo, Alihesabiwa pamoja na maasi.


Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.


Akajihu akawaambia, Ni kweli Eliya yuaja kwanza, na kutengeneza yote; lakini, pamoja na haya ameandikwaje Mwana wa Adamu ya kwamba atateswa mengi na kudharanliwa?


Marra baba yake yule kijana akapaaza sauti, machozi yakimtoka, akanena, Naamini, Bwana, nisaidie kutokuamini kwangu.


Mitume wakamwambia, Bwana, utuongezee imani yetu.


Bassi Herode akamtweza pamoja na askari zake akamdhihaki, akamvika mavazi mazurimazuri, akamrudisha kwa Pilato.


Haikumpasa Kristo kupata mateso haya, ndipo aingie enzini mwake?


Siku ya pili yake Yohana amwona Yesu anakuja kwake, akanena, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuae dhambi ya ulimwengu!


Amin, amin, nawaambieni, Punje ya nganu isipoanguka katika inchi ikafa, hukaa katika hali ya peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.


Nami nikiinuliwa juu ya inchi nitavuta wote kwangu.


bassi Yesu akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu, na anakwenda kwa Mungu,


Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya ya kwamba killa amtazamae Mwana na kumwamini awe ua uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.


Ibrahimu baba yemi alishangilia apate kuiona siku yangu; akaona, akafurahi.


Bassi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.


mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambae Mungu amemfufua: na sisi tu mashahidi wake.


Mtu kuyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toha na masamaha ya dhambi.


Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya jina lake.


Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.


bali sisi tunamkhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upumbavu,


na kuwapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa msalaba, akiisha kuuua ule uadui kwa huo msalaba;


mkaenende katika upendo, kama na Kristo alivyowapenda ninyi, akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu nzuri.


niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hatta siku ya Yesu Kristo;


Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbiuguni; kutoka huko tena tunamtazamia mwokozi Bwana Yesu Kristo;


baada ya haya nimewekewa taji ya baki, ambayo Bwana mhukumu wa haki atanipa katika siku ile: wala si mimi tu, bali watu wote pia waliopenda kutokea kwake.


Je! yuko malaika aliyeambiwa nae maneno haya wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume hatta nitakapoweka adui zako chiui ya nyayo zako?


Yeye kwa kuwa ni mwanga wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivitengeneza vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya peke yake utakaso wa dhambi zetu, aliketi juu mkono wa kuume wa ukuu;


Maana kwa toleo moja amewakamilisha hatta milele wanaotakaswa.


pindi mlipotwezwa kwa mashutumu na mateso, na pindi mliposhirikiana na wale waliotendewa hayo.


wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani:


Maana mtafakarini sana yeye aliyeyavumilia mapingamizi makuu namna hii ya wenye dhambi juu ya nafsi zao, msije mkadhoofika mkizimia mioyoni mwenu.


Bassi na twende kwake nje ya kituo, tukichukua laumu lake.


nae alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokofu wa milele kwa watu wote wanaomtii;


(kwa maana sharia ile haikukamilisha neno); na pamoja na haya kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwayo twamkaribia Mungu.


BASSI, katika hayo tuuayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunae kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu mbinguni,


kadhalika Kristo, akiisha kutolewa sadaka marra moja aziondoe dhambi za watu wengi, marra ya pili, pasipo dhambi, ataonekana nao wamtazamiao kwa wokofu.


NDUGU zangu, msiwe na imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana mwenye utukufu, kwa kupendelea watu.


wakitafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho ya Kristo iliyokuwa ndaui yao, aliyetangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwa baada ya hayo.


Kwa maana Kristo nae aliteswa marra moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio baki, illi atulete kwa Mungu; mwili wake akifishwa, bali roho yake akihuishwa.


alioko mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zimetiishwa chini yake.


jilindeni katika upendo wa Mungu, mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Krislo, hatta mpate uzima wa milele.


ikinena, Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Haya uonayo yaandike katika chuo, ukayapeleke kwa makanisa saba yaliyo katika Asia; Efeso, na Smurna, na Pergamo, na Thuatera, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.


Na nilipomwona nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akiniambia, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,


Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisiio, asema Bwana Mungu, alioko, aliyekuwako, na atakaekuwako, Mwenyiezi.


Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Smurna andika; Haya ayanena yeye aliye wa kwanza na wa mwisbo, aliyekuwa amekufa, akawa hayi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo