Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 12:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua watu wengi, wakatiwe najis kwa hilo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Jitahidini sana mtu yeyote asije akapoteza neema ya Mungu. Muwe waangalifu ili mti mchungu usizuke kati yenu na kuwaua wengi kwa sumu yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Jitahidini sana mtu yeyote asije akapoteza neema ya Mungu. Muwe waangalifu ili mti mchungu usizuke kati yenu na kuwaua wengi kwa sumu yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Jitahidini sana mtu yeyote asije akapoteza neema ya Mungu. Muwe waangalifu ili mti mchungu usizuke kati yenu na kuwaua wengi kwa sumu yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Chungeni sana mtu yeyote asiikose neema ya Mungu, na kwamba shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Angalieni sana mtu yeyote asiikose neema ya Mwenyezi Mungu na kwamba shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.

Tazama sura Nakili




Waebrania 12:15
41 Marejeleo ya Msalaba  

lakini nimekuombea, illi imani yako isipunguke; nawe uongokapo, wathubutishe ndugu zako.


Bassi anaejidhani amesimama aangalie asianguke.


Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.


Msidanganyike: mazumgumzo mabaya huharibu tabia njema.


Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulitia chachu donge zima?


Jijaribuni nafsi zenu kwamba m katika imani; jithubutisheni nafsi zenu. Au bamjijui nafsi zenu, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu isipokuwa mmekataliwa?


NASI tukitenda kazi pamoja nae tunakusihini msiipokee neema ya Mungu burre,


Na Wayahudi wakajigeuza pamoja nae, hatta Barnaba nae akachukuliwa na unafiki wao.


Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kufanyiziwa wema kwa sharia; mmeanguka toka hali ya neema.


Lakini uasharati na uchafu wote au kutamani kusinenwe kwenu kabisa, kama iwastahilivyo watakatifu;


Bassi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika inchi, uasharati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu:


Vitu vyote ni sali kwao walio safi: lakini hapana kilicho safi kwa walio najis, wasioamini, bali akili zao na nia zao pia zimekuwa najis.


Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hayi.


BASSI, ikiwa ikaliko abadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.


Bassi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, mtu ye yote asije akaanguka kwti mfano huo huo wa kuasi.


Nasi twataka killa mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hatta mwisho;


Kwa hivo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara wito wenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.


wakinena maneno ya kiburi makuu mno, kwa tamaaza mwili na kwa uasharati huwakhadaa watu waliokwisha kuwakimbia wao waishio katika udanganyifu:


Bassi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na ntawa,


Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia hayo, fanyeni bidii illi muonekane kuwa hamna mawaa au aibu mbele yake, katika amani.


Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo