Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 11:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu ampendezae Mungu lazima aamini kwamba yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa maana kila mtu anayemwendea Mungu ni lazima aamini kwamba Mungu yuko, na kwamba huwatuza wale wanaomtafuta.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa maana kila mtu anayemwendea Mungu ni lazima aamini kwamba Mungu yuko, na kwamba huwatuza wale wanaomtafuta.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Basi, pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kwa maana kila mtu anayemwendea Mungu ni lazima aamini kwamba Mungu yuko, na kwamba huwatuza wale wanaomtafuta.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana yeyote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wanaomtafuta kwa bidii.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana yeyote anayemjia Mwenyezi Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii.

Tazama sura Nakili




Waebrania 11:6
47 Marejeleo ya Msalaba  

Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele yako.


Furahini, shangilieni: kwakuwa thawabu yenu nyingi mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu.


Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana: maana hujiumbua nyuso zao, illi waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambieni, wamekwisha kupata thawabu yao.


Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki yake; na haya yote mtazidishiwa.


Tena usalipo, usiwe kama wanafiki: kwa maana wapenda kusali wakisimama katika sunagogi na katika pembe za njia, illi waonekane na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao.


Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; Kwa jina langu watafukuza pepo; watasema kwa ndimi mpya;


Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na haya yote mtazidishiwa.


Bali wapendeni adui zenu, katendeni kwa ihsani, kopeshani, bali kutumaini kupata kitu tena: na thawabu yenu itakuwa nyingi, na mtakuwa wana wa Aliye juu sana; kwa sabahu Yeye yu mwema kwa watu wasio na shukrani, na waovu.


Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.


Bassi naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa kuwa msipoamini ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu.


Bassi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mkhubiri?


Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.


akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mwingi kuliko hazina za Misri.


Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hayi.


Maana ni kweli, sisi nasi tumekhubiriwa khabari njema kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa bao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.


Bassi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia, na wale waliokhubiriwa khabari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao,


(kwa maana sharia ile haikukamilisha neno); na pamoja na haya kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwayo twamkaribia Mungu.


Nae, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye; maana yu hayi siku zote illi awaombee.


Kwa hivo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara wito wenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.


Naam, na kwa sababu hiyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenn tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,


Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia hayo, fanyeni bidii illi muonekane kuwa hamna mawaa au aibu mbele yake, katika amani.


Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo