Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 11:36 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

36 wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

36 Wengine walidhihakiwa na kupigwa mijeledi, na wengine walifungwa minyororo na kutupwa gerezani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

36 Wengine walidhihakiwa na kupigwa mijeledi, na wengine walifungwa minyororo na kutupwa gerezani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

36 Wengine walidhihakiwa na kupigwa mijeledi, na wengine walifungwa minyororo na kutupwa gerezani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

36 Wengine walidhihakiwa na kupigwa, hata walifungwa minyororo na kutiwa gerezani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

36 Wengine walidhihakiwa na kupigwa, hata walifungwa minyororo na kutiwa gerezani.

Tazama sura Nakili




Waebrania 11:36
45 Marejeleo ya Msalaba  

na watampeleka kwa Mataifa wapate kumdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumsulibi; na siku ya tatu atafufuka.


Wale wakulima wakawakamata watumishi wake, huyu wakampiga, na mwingine wakamwua, na mwingine wakampiga mawe.


Kwa sababu hii, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi: na wengine wao mtawaua na mtawasulibi, na wengine wao mtawapiga katika sunagogi zenu, na mtawafukuza mji kwa mji;


Ndipo akawafungulia Barabba: na alipokwisha kumpiga Yesu mijeledi, akamtoa apate kusulibiwa.


na watamhukumu afe, watamtia mikononi mwa mataifa, nao watamdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumtemea mate, na kumwua: na siku ya tatu atafufuka.


Kwa maana atatiwa katika mikono ya Mataifa, atafanyiwa dhihaka na kutendwa jeuri, na kutemewa mate;


Bassi Herode akamtweza pamoja na askari zake akamdhihaki, akamvika mavazi mazurimazuri, akamrudisha kwa Pilato.


Askari wakamdhihaki, wakimjia, wakimpa siki, na kusema,


Kiisha jemadari akakaribia, akamshika, akaamuru afungwe kwa minyororo miwili: akauliza, Nani huyu? tena, amefanya nini?


Na miaka miwili ilipotimia. Feliki akampokea Porkio Festo atawale badala yake. Na Feliki, akitaka kuwafanyia Wayahudi fadhili, akamwacha Paolo amefungwa.


Wakawakamata, wakawaweka garezani hatta assubuhi; kwa kuwa imekwisha kuwa jioni.


wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza;


Wakakubali maneno yake; wakawaita mitume, wakawapiga, wakawaamuru wasinene kwa jina lake Yesu; kiisha wakawaacha waende zao.


Saul akaliharibu kanisa, akiingia killa nyumba, na kuwabarura wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.


KWA sababu biyo mimi Paolo, mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa,—


BASSI nawasihini, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa,


Bwana awape rehema walio wa uyumba ya Onesiforo; maana marra nyingi aliniburudisha, wala hakuutahayarikia mnyororo wangu;


Katika huyu nimeteswa kiasi cha kufungwa, kama mtenda mabaya; illakini neno la Mungu halifungwi.


Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika mafungo, mkakubali kwa furaba kunyangʼauywa mali zenu, mkijua nafsini mwenu kwamba mna mali mbinguni iliyo njema zaidi, idumnyo.


Usiogope mambo yatakavokupata: tazama mshitaki atawatupa baadhi yenu gerezani illi mjaribiwe, nanyi mtakuwa na mateso siku kumi. Uwe mwaminifu hatta kufa, nami nitakupa taji ya uzima.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo