Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 11:27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

27 Kwa imani akatoka Misri, asiogope hasira ya mfalme; maana alistahimili kama amwonae yeye asiyeonekana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Kwa imani Mose alihama kutoka nchi ya Misri bila kuogopa hasira ya mfalme; na wala hakurudi nyuma, kwani alikuwa kama mtu aliyemwona yule Mungu asiyeonekana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Kwa imani Mose alihama kutoka nchi ya Misri bila kuogopa hasira ya mfalme; na wala hakurudi nyuma, kwani alikuwa kama mtu aliyemwona yule Mungu asiyeonekana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Kwa imani Mose alihama kutoka nchi ya Misri bila kuogopa hasira ya mfalme; na wala hakurudi nyuma, kwani alikuwa kama mtu aliyemwona yule Mungu asiyeonekana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Kwa imani Musa aliondoka Misri bila kuogopa ghadhabu ya mfalme. Alivumilia kwa sababu alimwona yeye asiyeonekana kwa macho.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Kwa imani Musa aliondoka Misri bila kuogopa ghadhabu ya mfalme. Alivumilia kwa sababu alimwona yeye asiyeonekana kwa macho.

Tazama sura Nakili




Waebrania 11:27
27 Marejeleo ya Msalaba  

Na mtakuwa mkichukiwa na watu wole kwa ajili ya jina langu: lakini adumuye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka.


Lakini astahimiliye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka.


Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kustahimili hatta mwisho, ndiye atakaeokoka.


waki hawana mizizi ndani yao, hali hudumu muda mehache; kiisha ikitokea shidda au udhia kwa sababu ya lile neno, marra huchukizwa.


Maana Daud amtaja khabari zake, Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko mkono wangu wa kuume, nisitikisike.


hustahimili yote, huamini yote, hutumaini yote, huvumilia yote.


tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.


nae ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.


Kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu wa hekima peke yake, kwake yeye heshima na utukufu milele na milele. Amin.


ambae yeye peke yake hapatikani na mauti, akaae katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hapana mwana Adamu aliyemwona, wala awezae kumwona, ndiye mwenye heshima na uweza milele. Amin.


Lakini zikumbukeni siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu;


BASSI imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.


Hawa wote wakafa katika imani, wasizipokee zile ahadi, bali wakiziona tokea mbali na kuzisalimu, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya inchi.


Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi.


Angalieni, twawaita wenye kheri wao waliovumilia. Mmesikia khabari ya uvumilivu wa Ayub, mmenona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwenye rehema nyingi, mwenye huruma.


ambae mwampenda, ijapokuwa hamkumwona: ambae ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini, na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, iliyotukuzwa,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo