Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 11:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Lakini sasa waitamani inchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Lakini sasa wanataka nchi iliyo bora zaidi, yaani nchi ya mbinguni. Ndio maana Mungu haoni haya wakimwita yeye Mungu wao, kwa sababu yeye mwenyewe amekwisha watayarishia mji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Lakini sasa wanataka nchi iliyo bora zaidi, yaani nchi ya mbinguni. Ndio maana Mungu haoni haya wakimwita yeye Mungu wao, kwa sababu yeye mwenyewe amekwisha watayarishia mji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Lakini sasa wanataka nchi iliyo bora zaidi, yaani nchi ya mbinguni. Ndio maana Mungu haoni haya wakimwita yeye Mungu wao, kwa sababu yeye mwenyewe amekwisha watayarishia mji.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Lakini badala yake walitamani nchi iliyo bora zaidi, yaani nchi ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni aibu kuitwa Mungu wao, kwa kuwa amekwisha kuandaa mji kwa ajili yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Lakini badala yake walitamani nchi iliyo bora zaidi, yaani nchi ya mbinguni. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu haoni aibu kuitwa Mungu wao, kwa kuwa amekwisha kuandaa mji kwa ajili yao.

Tazama sura Nakili




Waebrania 11:16
26 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha Mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa wa Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa ulimwengu:


Na katika khabari ya wafu ya kwamba wafufuka, hamjasoma katika Kitabu cha Musa, mwenye Kijiti, jinsi Mungu alivyomwambia, akinena, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaak, na Mungu wa Yakobo?


Maana killa mtu atakaenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha zina na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya yeye atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.


Msiogope, enyi kundi dogo, kwa kuwa Baba yenu ameona vyema kuwapeni ufalme.


Walakini ya kuwa wafu wafufuka, Musa nae alionyesha katika sura ya Kijiti, hapo amtajapo Bwana kuwa ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaak, na Mungu wa Yakobo.


Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambieni; nashika njia kwenda kuwaandalia mahali.


Mimi ni Mungu wa baba zako, Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaak, na Mungu wa Yakobo.


Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbiuguni; kutoka huko tena tunamtazamia mwokozi Bwana Yesu Kristo;


Na Bwana ataniokoa na killa neno baya na kunihifadhi hatta uje ufalme wake wa milele.


Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika mafungo, mkakubali kwa furaba kunyangʼauywa mali zenu, mkijua nafsini mwenu kwamba mna mali mbinguni iliyo njema zaidi, idumnyo.


Maana waliutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuujenga na kuufanyiza ni Mungu.


Maana wasemao maneno kama hayo waonyesha kwa wazi kwamba wanatafuta inchi yao wenyewe.


kwa kuwa Mungu ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, illi wasikamilishwe pasipo sisi.


Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye tiayi, Yerusalemi wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,


Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.


Maana yeye atakasae nao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;


Nami Yohana nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemi mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo