Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 11:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Kuwa na imani ni kuwa na hakika ya mambo tunayotumainia; kusadiki kabisa mambo tusiyoyaona.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Kuwa na imani ni kuwa na hakika ya mambo tunayotumainia; kusadiki kabisa mambo tusiyoyaona.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Kuwa na imani ni kuwa na hakika ya mambo tunayotumainia; kusadiki kabisa mambo tusiyoyaona.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, na udhahiri wa mambo yasiyoonekana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, na udhahiri wa mambo yasiyoonekana.

Tazama sura Nakili




Waebrania 11:1
24 Marejeleo ya Msalaba  

nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani toba iliyo kwa Mungu, na imani iliyo kwa Bwana wetu Yesu Kristo.


Bassi, sasa inabaki imani, tumaini, upendo, hizi tatu; na iliyo kuu katika hizi ni upendo.


Nisemalo silisemi agizo la Bwana, bali kama kwa upumbavu, katika ujasiri huu wa kujisifu.


tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.


Hatta imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo ni kiumbe kipya, vya kale vimepita; kumbe! vyote vimekuwa vipya.


Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.


kusudi, wakija Wamakedoni pamoja nami, na kuwakuta hamjawa tayari, tusije tukatahayarika sisi, tusiseme ninyi, katika hali hii va kutumaini.


Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.


PAOLO, mtumwa wa Mungu, mtume wa Yesu Kristo, illi ienee imani ya wateule wa Mungu, na ujuzi wa kweli iletayo utawa,


tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa mwili kwa maji safi.


Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali miongoni mwao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.


Hawa wote wakafa katika imani, wasizipokee zile ahadi, bali wakiziona tokea mbali na kuzisalimu, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya inchi.


Kwa imani akatoka Misri, asiogope hasira ya mfalme; maana alistahimili kama amwonae yeye asiyeonekana.


Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu khabari za mambo yasiyoonekana bado, kwa kumcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Kwa hiyo akauhukumu ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.


sisi je! tutapataje kujiponya, tusipotunza wokofu mkiju namna hii? ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kiisha nkathubutika kwetu na wale waliosikia;


Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu mpaka mwisho;


bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba yake; ambae nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na kujisifu kwetu, kwa kutumaini mpaka mwisho.


illi msiwe wavivu, hali wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imaui na uvumilivu.


SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo