Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 10:39 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

39 Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali miongoni mwao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

39 Basi, sisi hatumo miongoni mwa wale wanaorudi nyuma na kupotea, ila sisi tumo na wale wanaoamini na kuokolewa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

39 Basi, sisi hatumo miongoni mwa wale wanaorudi nyuma na kupotea, ila sisi tumo na wale wanaoamini na kuokolewa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

39 Basi, sisi hatumo miongoni mwa wale wanaorudi nyuma na kupotea, ila sisi tumo na wale wanaoamini na kuokolewa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

39 Lakini sisi hatumo miongoni mwa hao wanaositasita na kuangamia, bali tuko miongoni mwa hao wenye imani na hivyo tunaokolewa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

39 Lakini sisi hatumo miongoni mwa hao wanaositasita na kuangamia, bali tuko miongoni mwa hao wenye imani na hivyo tunaokolewa.

Tazama sura Nakili




Waebrania 10:39
28 Marejeleo ya Msalaba  

Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.


Marra huenda, huchukua pepo saba wengine walio waovu kupita nafsi yake: nao huingia na kukaa humo: na mambo ya mwisho ya mtu yule huwa mabaya kuliko ya kwanza.


Nilipokuwa pamoja nao ulimwenguni, mimi naliwalinda kwa jina lako: wale ulionipa naliwatunza, wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, illa yule mwana wa upotevu maandiko yapate kutimizwa.


lakini hizi zimeandikwa mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.


Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima.


Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya ya kwamba killa amtazamae Mwana na kumwamini awe ua uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.


Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira vake bali tupate wokofu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo,


Mtu aliye yote asiwadanganye kwa njia yo yote, maana haiji isipokuja kwanza ile faraka, akafumiliwa yule mtu wa dhambi, mwana wa uharibifu,


Watakao kuwa na mali waanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa zisizo maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wana Adamu katika upotevu na uharibifu.


Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;


Lakini mwenye haki ataishi kwa imani; nae akisitasita, roho yangu haina furaha nae.


BASSI imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.


mnaolindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani mpate wokofu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.


Lakini mbingu za sasa na inchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hatta siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wana Adamn wasiomcha Mungu.


Mtu akimwona ndugu yake anakosa kosa lisilo la mauti, ataomba, nae atampa uzima kwa ajili ya hawo wakosao kosa lisilo la mauti. Liko kosa lililo la mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hilo.


Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa yeye aaminiye ya kwamba Yesu yu Mwana wa Mungu?


Na yule nyama aliyekuwako nae hayuko, yeye ndiye wa nane, nae ni mmoja wa wale saba, nae aenenda kwenye uharibifu.


Yule nyama uliyemwona alikuwako, nae hayuko, nae yu tayari kupanda katika abuso na kwenda kwenye uharibifu. Nao wakaao juu ya inchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watataajabu wamwonapo yule nyama, ya kwamba alikuwako, nae hayuko, nae atakuwako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo