Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 10:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika mafungo, mkakubali kwa furaba kunyangʼauywa mali zenu, mkijua nafsini mwenu kwamba mna mali mbinguni iliyo njema zaidi, idumnyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Mlishiriki mateso ya wafungwa na mliponyanganywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Mlishiriki mateso ya wafungwa na mliponyanganywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Mlishiriki mateso ya wafungwa na mliponyang'anywa mali yenu mlistahimili kwa furaha, maana mlijua kwamba mnayo mali bora zaidi na ya kudumu milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Mliwahurumia wale waliokuwa kifungoni, mkikubali kwa furaha kunyang’anywa mali yenu kwa maana mlijua kwamba mnayo mali iliyo bora zaidi idumuyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Mliwahurumia wale waliokuwa kifungoni, mkikubali kwa furaha kunyang’anywa mali zenu kwa maana mlijua kwamba mnayo mali iliyo bora zaidi idumuyo.

Tazama sura Nakili




Waebrania 10:34
28 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze mali zako, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kiisha njoo unifuate.


lakini kuna haja ya kitu kimoja tu, na Mariamu ameichagua sehemu iliyo njema, ambayo hataondolewa.


Viuzeni mlivyo navyo, katoeni sadaka, jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, asikokaribia mwizi, wala nondo kuharibu.


Maana itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote na kujipoteza, au kupata khasara ya roho yake?


Kiisha jemadari akakaribia, akamshika, akaamuru afungwe kwa minyororo miwili: akauliza, Nani huyu? tena, amefanya nini?


Bassi kwa ajili ya hayo, nimewaiteni mje kunitazama na kusema nami; kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli.


Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya jina lake.


KWA maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia ikiharibiwa, tuna jengo litokalo kwa Mungu, nyumha isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele katika mbingu.


KWA sababu biyo mimi Paolo, mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa,—


BASSI nawasihini, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa,


kwayo ni mjumbe kifungoni; nipate ujasiri katika kunena jinsi nipaswavyo kusema.


kama ilivyo wajib wangu kufikiri haya juu yenu nyote; kwa sababu ninyi mmo moyoni mwangu; kwa kuwa katika kufungwa kwangu na katika kazi ya kuitetea Injili na kuithubutisha, ninyi nyote mmeshirikiana nami neema hii.


kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, khabari zake mlisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili;


wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao illi wapate uzima wa milele.


Bwana awape rehema walio wa uyumba ya Onesiforo; maana marra nyingi aliniburudisha, wala hakuutahayarikia mnyororo wangu;


Katika huyu nimeteswa kiasi cha kufungwa, kama mtenda mabaya; illakini neno la Mungu halifungwi.


baada ya haya nimewekewa taji ya baki, ambayo Bwana mhukumu wa haki atanipa katika siku ile: wala si mimi tu, bali watu wote pia waliopenda kutokea kwake.


Lakini sasa waitamani inchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.


Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.


Wakumbukeni waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao; nao wanaodhulumiwa, kwa kuwa nanyi m katika mwili.


Na kwa sababu hii yu mjumbe wa agauo jipya, illi, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa ya katika agano la kwanza, walioitiwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.


Hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, ndugu zangu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;


tupate urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu,


Wapenzi, sasa tu wana wti Mungu, wala haijadhihirika bado tutakidokuwa: lakini twajua ya kuwa akidhihiri, tutafanana nae; kwa maana tutamwona kama alivyo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo