Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 10:29 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa nayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho ya neema?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Je, mtu yule anayempuuza Mwana wa Mungu na kuidharau damu ya agano la Mungu iliyomtakasa, mtu anayemtukana Roho wa Mungu, anastahili kupata adhabu kali ya namna gani?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Je, mtu yule anayempuuza Mwana wa Mungu na kuidharau damu ya agano la Mungu iliyomtakasa, mtu anayemtukana Roho wa Mungu, anastahili kupata adhabu kali ya namna gani?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Je, mtu yule anayempuuza Mwana wa Mungu na kuidharau damu ya agano la Mungu iliyomtakasa, mtu anayemtukana Roho wa Mungu, anastahili kupata adhabu kali ya namna gani?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Je, mnadhani ni adhabu kali kiasi gani anayostahili kupewa mtu aliyemkanyaga Mwana wa Mungu chini ya nyayo zake, yeye aliyeifanya damu ya agano iliyomtakasa kuwa kitu najisi na kumtendea maovu Roho wa neema?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Je, mnadhani ni adhabu kali kiasi gani anayostahili kupewa mtu aliyemkanyaga Mwana wa Mungu chini ya nyayo zake, yeye aliyeifanya damu ya Agano iliyomtakasa kuwa kitu najisi na kumtendea maovu Roho wa neema?

Tazama sura Nakili




Waebrania 10:29
40 Marejeleo ya Msalaba  

maana hii ni damu yangu ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.


Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararueni.


wakaona baadhi ya wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najis, yaani, yasiyonawiwa, wakawalaumu.


Na killa mmoja atakaesema neno juu ya Mwana wa Adamu, atasamehewa, bali yeye aliyemtukana Roho Mtakatifu hatasamehewa.


je! yeye ambae Baba alimtakasa akamtuma ulimwenguni, ninyi mwamwambia, Unakufuru, kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?


Na kwa ajili yao najitakasa, illi na hawa watakaswe katika kweli.


Enyi wenye shingo gumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; kama baba zenu walivyofanya na ninyi vivyo hivyo.


Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu kwa upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.


Bassi killa aulae mkate huu, au kunywea kikombe hiki, asivyostahili, atakuwa amejipatia khatiya kwa ajili ya mwili na damu ya Bwana.


Maana alae na kunywa asivyostahili, hula na hunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua mwili wa Bwana.


Maana sharti amiliki yeye, hatta awaweke maadui wote chini ya miguu yake.


Kwa kuwa alitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini akisema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hamo.


Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hizi; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa kuwa na haki katika jina la Bwana Yesu na katika Roho ya Mungu wetu.


Wala msimhuzunishe Roho yule Mtakatifu wa Mungu; kwa yeye mlitiwa muhuri mpaka siku ya ukombozi.


kusudi alitakase na kulisafisha kwa maji, na kwa Neno;


Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo marra moja.


Angalieni msimkatae yeye anenae. Maana ikiwa wale hawakuokoka waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya inchi, sembuse sisi tukijiepusha nae atuonyae kutoka mbinguni:


Bassi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka wafu Mchungaji wa kondoo aliye mkuu, kwa damu ya agano la milele, Bwana wetu Yesu,


Maana yeye atakasae nao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;


sisi je! tutapataje kujiponya, tusipotunza wokofu mkiju namna hii? ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kiisha nkathubutika kwetu na wale waliosikia;


Bassi, iwapo tunae kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, tujashike sana maungamo yetu.


Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,


wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hatta wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu marra ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.


Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ngʼombe waliyonyunyizwa wenye uchafu hutakasa hatta kuutakatisha mwili;


akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu.


na zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi alive mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Kwake yeye aliyetupeuda na kutuosha dhambi zetu kwa damu yake,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo