Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 10:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa mwili kwa maji safi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Kwa hiyo tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu na imani timilifu, kwa mioyo iliyotakaswa kutokana na dhamiri mbaya, na kwa miili iliyosafishwa kwa maji safi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Kwa hiyo tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu na imani timilifu, kwa mioyo iliyotakaswa kutokana na dhamiri mbaya, na kwa miili iliyosafishwa kwa maji safi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Kwa hiyo tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu na imani timilifu, kwa mioyo iliyotakaswa kutokana na dhamiri mbaya, na kwa miili iliyosafishwa kwa maji safi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 sisi na tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu kwa imani timilifu, mioyo yetu ikiwa imenyunyizwa damu ya Al-Masihi na kuwa safi kutokana na dhamiri mbaya nayo miili yetu ikiwa imeoshwa kwa maji safi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 sisi na tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu kwa imani timilifu, mioyo yetu ikiwa imenyunyizwa damu ya Al-Masihi na kuwa safi kutokana na dhamiri mbaya nayo miili yetu ikiwa imeoshwa kwa maji safi.

Tazama sura Nakili




Waebrania 10:22
66 Marejeleo ya Msalaba  

Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.


KWA kuwa wiitu wengi wametia mkono kutunga khabari za mambo yale yaliyotimizwa kati yetu,


Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.


Nao, waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianza tangu wazee hatta wa mwisho; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke akisimama katikati.


Bassi sasa, unakawiliani? Simama ubatizwe ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina la Bwana.


Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele ya Mungu.


Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hizi; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa kuwa na haki katika jina la Bwana Yesu na katika Roho ya Mungu wetu.


BASSI, kwa kuwa tuna ahadi hizo, wapenzi, tujitakase nafsi zelu uchafu wote wa mwili na roho, tukitimiza utakatifu katika kumeha Mungu.


Katika yeye tuna ajasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya imani yake.


kusudi alitakase na kulisafisha kwa maji, na kwa Neno;


Watumwa, watiini walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili kana kwamba ni kumtii Kristo, kwa khofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo,


kwa unafiki wa watu wasemao uwongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;


alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda, bali kwa rehema yake, kwa josho la kuzaliwa kwa pili, na kufanywa upya na Roho Mtakatifu,


BASSI kwa kuwa torati ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo, kwa dhahihu zile zile wanazozitoa killa mwaka daima, hawawezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.


Bassi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu,


Kwa imani akaifanya Pasaka, na kunyunyiza ile damu, illi mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao.


na Yesu mwenye kuleta agano jipya, na damu ya kunyunyizwa inenayo mema kuliko ile ya Habil.


Bassi na tukikaribie kiti cha neema kwa nthubuitifu, illi tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.


Nasi twataka killa mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hatta mwisho;


(kwa maana sharia ile haikukamilisha neno); na pamoja na haya kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwayo twamkaribia Mungu.


kwa kuwa ni sharia za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hatta wakati wa matengenezo mapya.


Maana killa amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa watu wote, kama ilivyoamuru sharia, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi pamoja na maji na sufu nyekundu na husopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote,


Illa aombe kwa imani, pasipo shaka lo lote; maana mwenye mashaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa kwa upepo, na kupeperushwa huko na huko.


Mkaribieni Mungu, nae atsiwakaribieni ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, kaisafisheni mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.


kama vile Mungu alivyotangulia kuwajua tangu milele katika utakaso wa Roho, hatta wakapata kutii na kunyunyizwa damu ya Yesu Kristo; Neema na amani ziongezwe kwenu.


Mfano wa mambo haya ni ubatizo, nnaowaokoa na ninyi siku hizi; (sio kuwekea, mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo;


na zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi alive mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Kwake yeye aliyetupeuda na kutuosha dhambi zetu kwa damu yake,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo