Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 10:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hatta milele wanaotakaswa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Basi, kwa tambiko yake moja, amewafanya kuwa wakamilifu milele wote wale wanaotakaswa dhambi zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Basi, kwa tambiko yake moja, amewafanya kuwa wakamilifu milele wote wale wanaotakaswa dhambi zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Basi, kwa tambiko yake moja, amewafanya kuwa wakamilifu milele wote wale wanaotakaswa dhambi zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 kwa sababu kwa dhabihu moja amewafanya wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 kwa sababu kwa dhabihu moja amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa.

Tazama sura Nakili




Waebrania 10:14
16 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, sasa ndugu, nawawekeni katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, kwake yeye awezae kuwajengeni na kuwapeni urithi pamoja nao wote waliotakasika.


Ee Mfalme, wakati wa adhdhuhuri njiani naliona nuru inatoka mbinguni ipitayo mwangaza wa jua, ikinimulikia mimi, na wale waliofuatana nami pande zote.


illi niwe kuhani wa Yesu Kristo katika watu wa mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.


kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, lililotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo killa mahali, Bwana wao na wetu:


kusudi alitakase na kulisafisha kwa maji, na kwa Neno;


BASSI kwa kuwa torati ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo, kwa dhahihu zile zile wanazozitoa killa mwaka daima, hawawezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.


Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo marra moja.


Lakini huyu, alipokwisha kutoa dhabihu nioja kwa dhambi, idumuyo hatta milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu;


Kwa ajili hii Yesu nae, illi awatakase watu wake kwa damu yake miwenyewe, alitesyia nje ya mlango.


Maana yeye atakasae nao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;


(kwa maana sharia ile haikukamilisha neno); na pamoja na haya kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwayo twamkaribia Mungu.


Nae, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye; maana yu hayi siku zote illi awaombee.


kwa kuwa ni sharia za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hatta wakati wa matengenezo mapya.


bassi si zaidi damu yake Kristo, ambae kwamba kwa Roho ya milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo mawaa, itawasafisheni dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hayi?


YUDA, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu wa Yakobo, kwao waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo baada ya kuitwa;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo