Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 10:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Lakini huyu, alipokwisha kutoa dhabihu nioja kwa dhambi, idumuyo hatta milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Lakini Kristo alitoa tambiko moja kwa ajili ya dhambi, tambiko ifaayo milele, kisha, akaketi upande wa kulia wa Mungu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Lakini Kristo alitoa tambiko moja kwa ajili ya dhambi, tambiko ifaayo milele, kisha, akaketi upande wa kulia wa Mungu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Lakini Kristo alitoa tambiko moja kwa ajili ya dhambi, tambiko ifaayo milele, kisha, akaketi upande wa kulia wa Mungu,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Lakini huyu kuhani baada ya kutoa dhabihu moja kwa ajili ya dhambi kwa wakati wote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Lakini huyu kuhani akiisha kutoa dhabihu moja kwa ajili ya dhambi kwa wakati wote, aliketi mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili




Waebrania 10:12
15 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.


Ni nani atakaewahukumu? Kristo ndiye aliyekufa, naam, na zaidi ya haya, amefufuka, nae yuko mkono wa kuume wa Mungu, tena ndiye anaetuombea.


mkaenende katika upendo, kama na Kristo alivyowapenda ninyi, akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu nzuri.


BASSI mkiwa mmefufuka panioja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko mkono wa kuume wa Mungu, ameketi.


Yeye kwa kuwa ni mwanga wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivitengeneza vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya peke yake utakaso wa dhambi zetu, aliketi juu mkono wa kuume wa ukuu;


Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo marra moja.


Maana kwa toleo moja amewakamilisha hatta milele wanaotakaswa.


MAANA killa Kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wami Adamu amewekwa kwa ajili ya wana Adamu katika mambo yamkhusuyo Mungu, illi atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi;


na kwa sababu hiyo imempasa, kama kwa ajili ya watu, vivyo hivyo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi.


asiye na baja killa siku, kwa mfano wa wale makuhani wakuu wengine, kwanza kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kiisha kwa ajili ya dhambi za watu; maana yeye alifanya hivi marra moja, alipojitoa nafsi yake.


BASSI, katika hayo tuuayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunae kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu mbinguni,


wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia marra moja katika patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.


bassi si zaidi damu yake Kristo, ambae kwamba kwa Roho ya milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo mawaa, itawasafisheni dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hayi?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo