Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 10:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI kwa kuwa torati ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo, kwa dhahihu zile zile wanazozitoa killa mwaka daima, hawawezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Kwa vile sheria ni kivuli tu cha mambo mema yatakayokuja na si picha kamili ya mambo yale halisi, tambiko zilezile za sheria zinazotolewa mwaka hata mwaka, haziwezi kamwe kuwafanya wale wanaoabudu wawe wakamilifu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Kwa vile sheria ni kivuli tu cha mambo mema yatakayokuja na si picha kamili ya mambo yale halisi, tambiko zilezile za sheria zinazotolewa mwaka hata mwaka, haziwezi kamwe kuwafanya wale wanaoabudu wawe wakamilifu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Kwa vile sheria ni kivuli tu cha mambo mema yatakayokuja na si picha kamili ya mambo yale halisi, tambiko zilezile za sheria zinazotolewa mwaka hata mwaka, haziwezi kamwe kuwafanya wale wanaoabudu wawe wakamilifu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Torati ni kivuli tu cha mambo mema yajayo, wala si uhalisi wa mambo yenyewe. Kwa sababu hii, haiwezekani kamwe kupitia kwa dhabihu zitolewazo mwaka hadi mwaka kuwakamilisha wale wanaokaribia ili kuabudu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Torati ni kivuli tu cha mambo mema yajayo, wala si uhalisi wa mambo yenyewe. Kwa sababu hii, haiwezekani kamwe kwa njia ya dhabihu zitolewazo mwaka hadi mwaka kuwakamilisha wale wanaokaribia ili kuabudu.

Tazama sura Nakili




Waebrania 10:1
13 Marejeleo ya Msalaba  

Maana yale yasiyowezekana kwa sharia, kwa kuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa ajili ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili:


mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.


tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa mwili kwa maji safi.


Bassi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi: (maana watu wale waliipata sharia kwa huo) kulikuwa na haja gani tena kuhani mwingine aondoke, wa daraja la Melkizedeki, wala si kwa daraja la Haruni?


watumikao kwa mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile khema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.


Lakini Kristo akiisha kuwapo, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwa, kwa khema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu,


Bassi sharti manukulu ya mambo yaliyo mbinguni yasafishwe kwa haya, lakini mambo ya mbinguni yenyewe kwa dhabibu zilizo bora kuliko haya.


wala si kusudi ajitoe marra nyiugi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo patakatifu killa mwaka kwa damu isiyo yake;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo