Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 1:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Umependa haki, umechukia maasi: kwa sababu hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, mafuta ya shangwe kupita wenzako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Wewe wapenda uadilifu na kuchukia uovu. Ndiyo maana Mungu, Mungu wako, amekuweka wakfu na kukumiminia furaha kubwa kuliko wenzako.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Wewe wapenda uadilifu na kuchukia uovu. Ndiyo maana Mungu, Mungu wako, amekuweka wakfu na kukumiminia furaha kubwa kuliko wenzako.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Wewe wapenda uadilifu na kuchukia uovu. Ndiyo maana Mungu, Mungu wako, amekuweka wakfu na kukumiminia furaha kubwa kuliko wenzako.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Umependa haki na kuchukia uovu; kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekuweka juu ya wenzako kwa kukupaka mafuta ya furaha.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Umependa haki na kuchukia uovu; kwa hiyo Mungu Mwenyezi, Mungu wako, amekuweka juu ya wenzako kwa kukupaka mafuta ya furaha.”

Tazama sura Nakili




Waebrania 1:9
42 Marejeleo ya Msalaba  

Roho ya Bwana ni juu yangu, Kwa sababu amenitia mafuia kuwakhubiri maskini khabari njema. Amenituma kuwaponya waliopondeka moyo, Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa, na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha wa huru waliosetwa,


Huyu akamwona kwanza Simon, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi, (tafsiri yake Kristo).


Ndio maana Baba anipenda, kwa sababu nauweka uzima wangu illi niutwae tena.


Yesu akamwambia, Usiniguse; kwa maana sijapaa kwa Baba yangu. Lakini enenda kwa ndugu zangu, ukawaambie, Ninapaa kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu.


Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu: kwa sababu Mungu hampi Roho kwa kupima.


khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae.


Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja, Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake.


Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika juu ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,


Pendo niwe nalo pasipo unafiki; mkichukia lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.


Bassi Mungu wa tumaini awajazeni furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mataktifu.


Mungu ni mwaminifu, ambae mliitwa nae muingie katika ushirika wa Mwana wake, Yesu Kristo Bwana wetu.


Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliye mtukufu hatta milele, ajua va kuwa sisemi nwongo.


Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


Atukuzwe Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani ya Kristo;


Kwa hiyo tena Mungu akamtukuza mno, akamkarimia Jina lile lipitalo killa jina;


Maana yeye atakasae nao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;


illa twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, illi kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya killa mtu.


Maana ilipendeza sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii, aliye mtakatifu, asiokuwa na uovu, asiokuua na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;


Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambae kwa rehema zake nyingi alituzaa marra ya pili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuliwa kwake Yesu Kristo,


tuliyoiona na kuisikia, twawakhubiri ninyi; ninyi nanyi mpate kushirikiana na sisi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.


Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolaiti, niyachukiayo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo