Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waebrania 1:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 KWA sehemu nyingi na kwa namna nyingi Mungu zamani alisema na babu zetu katika manabii,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Hapo zamani, Mungu alisema na babu zetu mara nyingi kwa namna nyingi kwa njia ya manabii,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Hapo zamani, Mungu alisema na babu zetu mara nyingi kwa namna nyingi kwa njia ya manabii,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Hapo zamani, Mungu alisema na babu zetu mara nyingi kwa namna nyingi kwa njia ya manabii,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Zamani, Mungu alisema na baba zetu kupitia kwa manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Zamani Mwenyezi Mungu alisema na baba zetu kwa njia ya manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali,

Tazama sura Nakili




Waebrania 1:1
35 Marejeleo ya Msalaba  

(Kwa jinsi alivyowaambia baba zetu) Ibrahimu na nzao wake, hatta milele.


Illi kuwatendea rehema baba zetu, Na kukumbuka agano lake takatifu;


Akaanza toka Musa na manabii, akawafasiria katika maandiko yote mambo yaliyomkhusu yeye.


Akawaambia, Haya ndiyo maneno yangu niliyowaambieni, nilipokuwa kwenu, ya kuwa hayana buddi kutimizwa yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii, na katika zaburi.


Lakini ajapo yeye, Roho ya kweli, atawaongozeni katika yote iliyo kweli: kwa maana hatasema kwa shauri lake yeye, lakini yote atakayosikia, atayasema, na mambo yajayo atawapasha khabari yake.


Kwa sababu hii Musa aliwapa tohara, si kwamba yatoka kwa Musa bali kwa babu zenu: nanyi siku ya sabato humtahiri mtu.


Sisi twajua ya kuwa Mungu alisema na Musa, bali huyo hatujui atokako.


Na sisi tunawakhubirieni ahadi ile waliyopewa baba zetu, ya kwamba Mungu ametutimizia sisi watoto wao ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu:


Bassi kwa kuwa nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake kwa jinsi ya kiwiliwili atamwinua Kristo, akae katika kiti chake cha enzi; yeye mwenyewe


Wakiislia kuwekana kwa siku, wakaja kwake nyumbani kwake, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sharia ya Musa na ya manabii, tangu assubuhi hatta jioni.


ambae ilimpasa kupokewa mbinguni hatta zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa vinywa vya manabii wake tokea mwanzo wa ulimwengu.


naam, yeye aliyeamhiwa, Katika Isaak uzao walio utaitwa,


Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa.


Angalieni msimkatae yeye anenae. Maana ikiwa wale hawakuokoka waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya inchi, sembuse sisi tukijiepusha nae atuonyae kutoka mbinguni:


Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na killa kosa na uasi ulipata ujira wa haki,


sisi je! tutapataje kujiponya, tusipotunza wokofu mkiju namna hii? ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kiisha nkathubutika kwetu na wale waliosikia;


Na Musa alikuwa mwaminifu katika nyumba yake yote kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa;


Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadae.


Vivyo hivyo Kristo nae hakujitukuza nafsi yake kufanywa Kuhani mkuu, lakini yeye aliyenena nae: Mwana wangu ni wewe, Mimi leo nimekuzaa:


Maana killa amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa watu wote, kama ilivyoamuru sharia, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi pamoja na maji na sufu nyekundu na husopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo