Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 9:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya inchi wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, illa wale watu wasio ua muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Wakaamrishwa wasiharibu nyasi za nchi wala majani wala miti yoyote, bali wawaharibu wale tu ambao hawakupigwa mhuri wa Mungu katika paji la uso.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Wakaamrishwa wasiharibu nyasi za nchi wala majani wala miti yoyote, bali wawaharibu wale tu ambao hawakupigwa mhuri wa Mungu katika paji la uso.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Wakaamrishwa wasiharibu nyasi za nchi wala majani wala miti yoyote, bali wawaharibu wale tu ambao hawakupigwa mhuri wa Mungu katika paji la uso.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Wakaambiwa wasidhuru majani ya nchi, wala mmea wala mti wowote, bali wawadhuru tu wale watu ambao hawana muhuri wa Mungu kwenye paji za nyuso zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Wakaambiwa wasidhuru nyasi ya nchi, wala mmea wala mti wowote, bali wawadhuru tu wale watu ambao hawana muhuri wa Mungu kwenye vipaji vya nyuso zao.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 9:4
15 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana wataondoka Makristo ya uwongo, na manabii ya uwongo, nao watafanyiza ishara kubwa ua mataajabu; wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wateule.


Wala msimhuzunishe Roho yule Mtakatifu wa Mungu; kwa yeye mlitiwa muhuri mpaka siku ya ukombozi.


NIKAONA, na tazama, Mwana kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arubaini na nne elfu pamoja nae, wenye jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.


Nikasikia sauti kati kati ya nyama wane wenye uhayi, ikisema, Kibaba cha nganu kwa nussu rupia, na vibaba vitatu vya shairi kwa nussu rupia, wala usiyadhuru mafuta na mvinyo.


BAADA ya haya nikaona malaika wane wamesimama katika pembe nne za inchi, wakizizuia pepo nne za inchi, upepo usivume juu ya inchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote.


Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyotangamana na damu, vikatupwa juu ya inchi: thuluth ya miti ikateketea, majani mabichi yote yakateketea.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo