Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 9:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue malaika wane waliofungwa kwenye mto mkubwa Eufrati.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Sauti hiyo ikamwambia huyo malaika wa sita mwenye tarumbeta, “Wafungulie malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Eufrate!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Sauti hiyo ikamwambia huyo malaika wa sita mwenye tarumbeta, “Wafungulie malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Eufrate!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Sauti hiyo ikamwambia huyo malaika wa sita mwenye tarumbeta, “Wafungulie malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Eufrate!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Ile sauti ikamwambia yule malaika wa sita mwenye tarumbeta, “Wafungulie wale malaika wanne waliofungwa kwenye ule mto mkubwa Frati.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Ile sauti ikamwambia yule malaika wa sita mwenye tarumbeta, “Wafungulie wale malaika wanne waliofungwa kwenye ule mto mkubwa Frati.”

Tazama sura Nakili

Ufunuo 9:14
12 Marejeleo ya Msalaba  

Malaika wa sita akakimimina kichupa chake juu ya mto ule mkubwa Eufrate, maji yake yakakauka illi njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.

BAADA ya haya nikaona malaika wane wamesimama katika pembe nne za inchi, wakizizuia pepo nne za inchi, upepo usivume juu ya inchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote.

Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hayi: akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wane waliopewa kuidhuru inchi na bahari,

Nikawaona malaika saba wasimamao mbele za Mungu, wakapewa baragumu saba.

Na wale malaika saba wenye baragumu saba wakajifanya tayari illi wazipige.

Wale malaika wane wakafunguliwa, waliowekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka illi waue thuluth ya wana Adamu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo