Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 8:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Malaika akakitwaa cheteso akakijaza moto wa madhbahu, akautupa juu ya inchi, kukawa sauti na radi na umeme na tetemeko la inchi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Kisha, malaika akakichukua hicho chetezo, akakijaza moto wa madhabahuni, akakitupa duniani. Kukawa na ngurumo, sauti, umeme na tetemeko la ardhi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Kisha, malaika akakichukua hicho chetezo, akakijaza moto wa madhabahuni, akakitupa duniani. Kukawa na ngurumo, sauti, umeme na tetemeko la ardhi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Kisha, malaika akakichukua hicho chetezo, akakijaza moto wa madhabahuni, akakitupa duniani. Kukawa na ngurumo, sauti, umeme na tetemeko la ardhi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Kisha yule malaika akakichukua kile chetezo, akakijaza moto kutoka kwa yale madhabahu, akautupa juu ya dunia. Pakatokea sauti za radi na ngurumo, miali ya radi na tetemeko la ardhi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Kisha yule malaika akachukua kile chetezo, akakijaza moto kutoka kwa yale madhabahu, akautupa juu ya dunia. Pakatokea sauti za radi, ngurumo, umeme wa radi na tetemeko la ardhi.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 8:5
24 Marejeleo ya Msalaba  

Maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwako na njaa, na maradhi, na matetemeko ya inchi pahali pahali.


Nimekuja kutupa moto duniani, na ukiwa umekwisha kuwashwa nataka nini zaidi?


Ghafula pakawa tetemeko kuu la inchi, hatta misingi ya gereza ikatikisika, na marra hiyo milango ikafunguka, vifungo vya watu wote vikalegezwa.


Hatta walipokwisha kumwomba Mungu, pahali paie walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa uthabiti.


Na katika saa ile palikuwa na tetemeko la inchi, nalo kubwa, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka, wana Adamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na khofu wakamtukuza Mungu wa mbingu.


Hekalu ya Mungu ikafunguliwa mbinguni na sanduku la agano likaonekana ndani ya hekalu yake. Kukawa umeme, na sauti, na radi, na tetemeko, na mvua ya mawe uyingi sana.


Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na ngurumo na sauti. Na taa saha za moto zikiwaka mbele ya kiti kile cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.


Nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, tazama, palikuwa tetemeko kuu la inchi, jua likawa jeusi kama gunia la nywele, mwezi ukawa kama damu,


Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhbahu, mwenye cheteso cha dhahabu, akapewa manukato mengi illi ayatie pamoja na sala za watakatifu juu ya madhbahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo