Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 8:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhbahu, mwenye cheteso cha dhahabu, akapewa manukato mengi illi ayatie pamoja na sala za watakatifu juu ya madhbahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Malaika mwingine akafika, anachukua chetezo cha dhahabu, akasimama mbele ya madhabahu ya kufukizia ubani. Naye akapewa ubani mwingi autoe sadaka pamoja na sala za watu wote wa Mungu juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Malaika mwingine akafika, anachukua chetezo cha dhahabu, akasimama mbele ya madhabahu ya kufukizia ubani. Naye akapewa ubani mwingi autoe sadaka pamoja na sala za watu wote wa Mungu juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Malaika mwingine akafika, anachukua chetezo cha dhahabu, akasimama mbele ya madhabahu ya kufukizia ubani. Naye akapewa ubani mwingi autoe sadaka pamoja na sala za watu wote wa Mungu juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Malaika mwingine, aliyekuwa na chetezo cha dhahabu, akaja na kusimama mbele ya madhabahu. Akapewa uvumba mwingi ili autoe pamoja na maombi ya watakatifu wote, juu ya yale madhabahu ya dhahabu yaliyo mbele ya kile kiti cha enzi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Malaika mwingine aliyekuwa na chetezo cha dhahabu, akaja na kusimama mbele ya madhabahu. Akapewa uvumba mwingi ili autoe pamoja na maombi ya watakatifu wote, juu ya yale madhabahu ya dhahabu yaliyo mbele ya kile kiti cha enzi.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 8:3
32 Marejeleo ya Msalaba  

Na mkutano wote wa watu walikuwa wakisali nje, saa ya kufukiza.


Ni nani atakaewahukumu? Kristo ndiye aliyekufa, naam, na zaidi ya haya, amefufuka, nae yuko mkono wa kuume wa Mungu, tena ndiye anaetuombea.


Nae, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye; maana yu hayi siku zote illi awaombee.


yenye cheteso cha dhahabu, na sanduku ya agano iliyofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye manna, na fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vibao vya agano;


NIKAONA malaika mwingine hodari akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake: na uso wake kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto.


Na malaika mwingine akatoka katika ile madhbabu, mwenye mamlaka juu ya moto; kwa sauti kuu akamlilia yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume matawi va mzabibu wa inchi, maana zabibu zake zimewiva sana.


Hatta alipokitwaa kile kitabu, nyama wane wenye uhayi na wale wazee ishirini na wane wakaanguka mbele ya Mwana Kondoo, killa mmoja wao ana kinubi, na vitupa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambavyo ni maombi ya watakatifu.


Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhbahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.


Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hayi: akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wane waliopewa kuidhuru inchi na bahari,


Na moshi wa yale manukato ukapanda pamoja na sala za watakatifu, katika mkono wa malaika, mbele za Mungu.


Malaika akakitwaa cheteso akakijaza moto wa madhbahu, akautupa juu ya inchi, kukawa sauti na radi na umeme na tetemeko la inchi.


Malaika wa sita akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka mbele za Mungu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo